NAY ASIMULIA ALIVYOMFICHA MAMA YAKE

NancyTheDreamtz
WAKATI ngoma yake ya Alisema ikitikisa kila kona kwa kuwa na mistari tata, msanii wa Muziki Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefungukia jinsi alivyomficha mama yake hadi alipoachia wimbo huo.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Nay alisema kuwa wakati anatengeneza hadi anaachia wimbo huo hakutaka mama yake ajue.


“Kiukweli nilifanya siri sikumueleza mama yangu kuhusu ule wimbo na mpaka natengeneza video yake sikumwambia lakini nilipokuwa studio nikawaza tu kwamba kuimba nyimbo za aina hii mama alishanikataza, huwa ananiambia niache kabisa kuimba kwa kuwa mimi nina watoto wananitegemea na familia kwa ujumla.

“Kwa kuwa nimlificha aliisikia mtaani akanipigia simu na kuniambia niende nyumbani, nilienda pale na kumkuta akinisubiri kwa hamu sana ili kuniuulizia kwa nini nimerudia tena kuimba? Ikabidi nimueleweshe tu sikuwa na jinsi akanielewa,” alisimulia Nay na kuongeza;
“Nilivyoutunga nikaishirikisha na menejimenti yangu nikaambiwa nimpe mwanasheria wangu aisikilize kwanza nikafanya hivyo alipoisikiliza akaniambia haina tatizo na vitu vichache tu nirekebishe nikafanya hivyo na hatimaye ikatoka.”
STORI: Neema Adrian.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele