Matokeo ya Taifa Stars Yamuibua Zitto ''Wachezaji Taifa Stars wasingeambiwa''

NancyTheDreamtz
Matokeo ya Taifa Stars Yamuibua Zitto ''Wachezaji Taifa Stars wasingeambiwa''
Mbunge wa Kigoma Mjini na mdau mkubwa wa michezo nchini Zitto Kabwe, amewatetea wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Cape Verde, kwa kusema wameumizwa na tukio la kutekwa kwa Mohammed Dewji.



Zitto kupitia mtandao wa Twitter ameweka ujumbe huo, akitamani wachezaji hao wasingepata taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mdau wa michezo nchini akiwa mlezi wa Simba SC.


Zitto Kabwe Ruyagwa

@zittokabwe
 Wachezaji wetu Taifa Stars wameumizwa sana na tukio la mwanamichezo mwenzao @moodewji kutekwa. Wengi walikuwa wanamjua in person na wengi zaidi wanachezea Timu anayoilea ya Simba Sports Club. I wish wasingeambiwa kabla Lakini dunia ya Habari hii. Ndugu zetu Polisi ONGEZA JUHUDI

8:58 PM - Oct 12, 2018
871
222 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy
Mo Dewji ambaye ni mwekezaji katika klabu ya soka ya Simba akimiliki asilimia 49 ya hisa za klabu ametekwa Alhamis Oktoba 11, 2018. Hadi sasa hajapatikana.

Taifa Stars jana usiku ulifungwa mabao 3-0 na wenyeji wao Cape Verde kwenye mchezo wa tatu wa kundi L, kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019     zitakazo fanyika nchini Cameroon.

Tanzania sasa inashika nafasi ya mwisho kwenye kundi L ikiwa na alama 2 sawa na Lesotho inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 2 lakini ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Uganda wapo kileleni wakifuatiwa na Cape Verde zote zikiwa na alama 4.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele