CHADEMA watangaza wagombea wao wa ubunge katika majimbo matatu yaliyoachwa wazi
CHADEMA wamefanya uteuzi wa majina matatu ya wagombea wao wa ubunge katika majimbo matatu yaliyoachwa wazi kutokana na hama hama ya vyama inayoendelea nchini.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Kikao Maalum cha Kamati Kuu iliyoketi kwa siku mbili, Agosti 15-16, mwaka huu, jijini Dar es Salaam baada ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa kuhusu chaguzi za marudio za ubunge na udiwani na hali ya kisiasa nchini;Kimefikia maazimio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo ya Monduli, Korogwe na Ukonga, watakaogombea kupitia CHADEMA kwenye uchaguzi wa marudio ambao kampeni zake zitaanza Agosti 24-Septemba 15 na siku ya kupiga kura ni Jumapili Septemba 16, mwaka huu.Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;1. Jimbo la Ukonga; Asia Daudi Msangi2. Jimbo la Korogwe; Amina Ally Saguti3. Jimbo la Monduli; Yonas Masiaya LaiserKamati Kuu ya Chama imefanya uteuzi huo wa wagombea ubunge kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2016, ibara ya 7.7.16(q).Maazimio mengine ya kikao hicho maalum cha Kamati Kuu ya Chama, yatatolewa katika hatua za baadae.Imetolewa leo Ijumaa, Agosti 17, 2018 na;Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Comments