Posts

China wadai huenda Virus vya Corona Vilienezwa na jeshi la USA

Image
NancyTheDreamtz    Na AFP AFISA wa cheo cha juu wa China amedai huenda jeshi la Amerika lilipeleka virusi hatari vya corona nchini humo huku maradhi hayo yakiendelea kuenea mataifa mbalimbali na kuua watu zaidi ya 5,000. Bila kufafanua, msemaji wa wizara ya ulinzi wa China, Zhao Lijian, aliandika kwenye Twitter kwamba, kuna uwezekano virusi hivyo vilipelekwa China na wanajeshi wa Amerika. Dai lake linawiana na habari zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii nchini China zikilaumu Amerika kwa mkurupuko huo. Mkuu wa kituo cha kudhibiti maradhi nchini China amesema, maradhi hayo yalianza soko la Wanyama katika jiji la Wuhan. Hata hivyo, maafisa wa China na wataalamu mashuhuri wa afya wanadai huenda virusi hivyo vilitoka kwingineko. China imefokea maafisa wa Amerika wanaoita maradhi hayo “virusi vya Wuhan.” Kwenye ujumbe wake wa Twitter, Zhao alipakia video ya mkuu wa kituo cha kuzuia maradhi cha Amerika akiwa mbele ya bunge la Congress akisema, baadhi ya r...

Z Anto akasirishwa na kauli za Wastara kwa Binti Kiziwi (Video)

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki, Z Anto amedai hajapendezwa na namna muigizaji Wastara waliivyokuwa akimzungumzia vibaya, Binti Kiziwi ambaye ameshiriki kama video queen kwenye wimbo wake ‘Nichape’ ambao kwa sasa unafanya vizuri. Hata hivyo muimbaji huyo ameshindwa kueleza mahusiano yake na Wastara.

Lema 'Ina Maana Mahakama imetoa CONTROL Number Mbili Kwa Ajili ya Malipo Mtu Mmoja?"

Image
Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema  ahoji ina maana mahakama inatoa control number mbili kwa ajili ya malipo ya mtu mmoja. “Unajua kuna level fulani ya maisha mtu ukifika hupaswi kabisa kuwa msanii! nauliza ata kama ni sawa je wanafikiri watafanikiwa nini,” alihoji Lema. Lema aliandika ujumbe unaosome hivi katika ukurasa wake wa Twitter “Kwamba Mahakama inatoa control number mbili kwa ajili ya malipo ya mtu mmoja? Unajua kuna level Fulani ya maisha mtu ukifika hupaswi kabisa kuwa msanii! nauliza ata kama ni sawa je wanafikiri watafanikiwa nini,”. Leo Rais John Magufuli amelimlipia faini mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa ambaye tupo gerezani kwa kushindwa kulipa fedha hizo baada ya kuhukumiwa katika kesi ya uchochozi akiwa na vigogo wenzake nane.

Maisha ya Msanii Hawa ni Darasa Tosha

Image
NancyTheDreamtz Msanii hawa aliyefahamika zaidi kupitia wimbo wa Diamond Plutinumz wa Nitarejea. Aliwahi kukiri kwamba stress za maisha zilimpelekea kuingia katika maisha ya utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na utumiaji wa pombe kali, bange na pombe za kienyeji (mataputapu) Hiyo ikapelekea kuuchukia wimbo wa nitarejea na kumlalamikia Diamond kwamba hakulipwa chochote kwenye wimbo wa Nitarejea. Kutokana na utumiaji wa pombe kali ikapelekea kuugua ugonjwa wa ini na kujaa sana kwa tumbo. Diamond akamsaidia kumpeleka India kwa ajili ya matibabu na akapona. Sasa hivi anaendelea na muziki. Ameachia wimbo mpya unaitwa Moyo ni wimbo mzuri; una maadili unaweza kuuangalia hata ukiwa na familia yako. Hii inatufundisha jinsi gani Mungu anatoa another chance Kwa ajli ya kujirekebisha. Sasa hivi Hawa anaoga, anapendeza. Kwa kifupi anajua kuimba. Simsifii sana.

Nafasi 21 za Ajira Zilizotangazwa Leo Tarehe 12 March 2020

Image
NancyTheDreamtz NAFASI za Ajira Zilizotangazwa Leo 12 March 2020 2 Job Opportunities at Tanzania Postal Bank READ More>> https://www.ajirayako.co.tz/2020/03/ajira_12.html Job Opportunity at Standard Bank - Officer, Strategic Sourcing READ More>> https://www.ajirayako.co.tz/2020/03/ajirayako_76.html Job Opportunity at Exim Bank - Card Manager READ More>> https://www.ajirayako.co.tz/2020/03/ajira_52.html Job Opportunity at Exim Bank - MI & Analytics Manager READ More >> https://www.ajirayako.co.tz/2020/03/ajira_11.html 3 Job Opportunities at The Community Development and Relief Trust (CODERT) READ More>> https://www.ajirayako.co.tz/2020/03/ajira_64.html Job Opportunity at Ongeza Tanzania Ltd - Senior Software Developer READ More>> https://www.ajirayako.co.tz/2020/03/ajira_27.html Job Opportunity at Umoja Tanzania Incorporated (Umoja) - English Teacher READ More>> https://www.ajirayak...

Yanga Yapigwa na KMC Bao 1-0, Yabaki Nafasi ya Tatu

Image
NancyTheDreamtz Timu ya Yanga imefungwa bao 1-0 dhidi ya KMC leo Machi 12, 2020 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mfungaji wa bao la KMC ni Salim Aiyee dakika ya 62.

Hukumu Ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA ni Leo Mahakama Ya Kisutu

Image
NancyTheDreamtz Mahakama ya Kisutu leo March 10, inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani hapo. Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018 na Hakimu ambaye sasa ni Jaji, Wilbard Mashauri. Mbali na Mbowe, wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Katibu Mkuu wa sasa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na mbunge, Halima Mdee. Wabunge wengine ni Esther Matiko, Esther Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche. Katika kesi hiyo, baadhi ya washtakiwa waliwekwa mahabusu kwa miezi mitatu kutokana na kukiuka masharti ya dhamana