PAUL Makonda "Dhuluma Ikimekidhiri Kwenye Ardhi, Tunafurahishwa na Ajicho Kifanya Jerry Slaa"

PAUL Makonda "Dhuluma Ikimekidhiri Kwenye Ardhi, Tunafurahishwa na Ajicho Kifanya Jerry Slaa" Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema kwa kiwango kikubwa dhuluma imekithiri Nchini na Watanzania wengi wameumizwa na dhuluma hususani katika sekta ya ardhi ambako imekithiri zaidi. Akiongea na Waandishi wa Habari leo Dar es salaam, Makonda amesema ———> “Dhuluma hii imegawanyika katika maeneo mengi au imegawanyika kwenye sekta nyingi na kama Chama tunao wajibu wa kuweka mkazo kwa kuisimamia na kuielekeza Serikali ili ipambane na dhuluma zinazowatesa na kuwaumiza Wananchi hasa walio wanyonge” “Ipo dhuluma kubwa sana kwenye sekta ya ardhi, huko kumekithiri, kilio cha Watu kunyang’anywa maeneo yao na wenye nguvu ya fedha imetawala, kilio cha Watu kupewa nyaraka au hati feki kimetawala na katika eneo hili tulitoa maelekezo mahususi tarehe 19 February 2024, kama Idara ya Itikadi na Mafunzo tunatiwa moyo na jitihada zinazochukuliwa na Waziri wetu wa Ardhi Jerry Slaa” nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele