Posts

Nilimpenda Sana Diamond, Ila Alinidharau: Zari The Boss Lady Amefunguka ...

Image
NancyTheDreamtz

PRINCESS TIFFAH JIBEBE VIDEO SNIPPET/Diamond Platnumz and Zari the Boss ...

Image
NancyTheDreamtz

Waziri Lugola sakata la Mo: Mtu anaweza tekwa kisa siasa, uchumi, mapenzi na njaa (Video)

Image
NancyTheDreamtz Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mfanyabiashara Mohamed Dewji na hadi sasa watu 20 wanashikiliwa kusaidia upelelezi. Waziri Lugola akizungumza na wanahabari amelitaka jeshi la polisi kufanya haraka katika upelelezi wake na kutomshikilia mtu kwa zaidi ya 24. Amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake. “Sababu za matukio ya kutekwa yanayotokea ni pamoja na kisiasa, kiuchumi, kimapenzi na njaa ili mtu apate fedha na sababu za kutekwa kwa Mohamed Dewji zitajulika hapo wahalifu watakapojulikana” Amesema Lugola.

Masaa 48 Yamepita Bado Mo Dewji Ajapatikana Baba yake aulizwa ishu ya simu ya mwanaye kuwa hewani

Image
NancyTheDreamtz Jeshi la Polisi bado linaendelea kumsaka mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Mohamed Dewji ‘Mo’ ikiwa ni zaidi ya saa 48 zimepita tangu atekwe nyara na watu wasiojulikana wakati akingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Hadi sasa mamlaka zinazohusika hazijatoa taarifa mpya kuhusu upatikanaji wa ‘Mo’. Ijumaa hii baba wa mfanyabiashara huyo, Gulam Dewji Hussein alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia taarifa zozote kuhusu mwanaye, alisema familia ilikuwa haijapata chochote kutoka polisi hadi jana jioni. Alipoulizwa kuhusu simu ya mwanaye inayosemekana ikipigwa inaita na kupokea ujumbe mfupi wa maandishi (sms), mzazi huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi asubiri kwa kuwa muda huo (wa jioni) alikuwa na wageni na asingeweza kuzungumzia suala hilo. Hata alipotafutwa baadaye hakuweza kupatikana.

Matokeo ya Taifa Stars Yamuibua Zitto ''Wachezaji Taifa Stars wasingeambiwa''

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa Kigoma Mjini na mdau mkubwa wa michezo nchini Zitto Kabwe, amewatetea wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Cape Verde, kwa kusema wameumizwa na tukio la kutekwa kwa Mohammed Dewji. Zitto kupitia mtandao wa Twitter ameweka ujumbe huo, akitamani wachezaji hao wasingepata taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mdau wa michezo nchini akiwa mlezi wa Simba SC. Zitto Kabwe Ruyagwa ✔ @zittokabwe  Wachezaji wetu Taifa Stars wameumizwa sana na tukio la mwanamichezo mwenzao @moodewji kutekwa. Wengi walikuwa wanamjua in person na wengi zaidi wanachezea Timu anayoilea ya Simba Sports Club. I wish wasingeambiwa kabla Lakini dunia ya Habari hii. Ndugu zetu Polisi ONGEZA JUHUDI 8:58 PM - Oct 12, 2018 871 222 people are talking about this Twitter Ads info and privacy Mo Dewji ambaye ni mwekezaji katika klabu ya soka ya Simba akimiliki asilimia 49 ya hisa za klabu ametekwa Alhamis Oktoba 11, 2018. Hadi...

Wapinzani DRC Watishia kuandamana kupinga mfumo wa upigaji kura

Image
NancyTheDreamtz Wagombea wakuu wa upinzani kwa nafasi ya urais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, upinzani umeitisha maandamano ya kupinga mfumo wa kura kwa mashine za elekroniki kwenye uchaguzi mkuu wa Desemba 23. Upinzani unasema kuwa wanapinga pia daftari la wapigakura wasio na alama za vidole kwenye kadi zao. Hata hivyo, Martin Fayulu, mmoja wa wagombea wa urais na ambaye alisoma taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani mbele ya waandishi wa habari mjini Kinshasa, alisema upinzani hauna nia ya kuususia uchaguzi huo. “Tunawatolea wito raia wa Kongo kujipanga kwa ajili ya kulazimisha kuweko na kura ya makaratasi kulingana na sheria ya uchaguzi na kalenda iliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi.” Licha ya hayo, wapinzani walisema wanaunga mkono juhudi zozote za mazungumzo ili kupata suluhisho kuhusu mfumo wa uchaguzi wa matumizi ya mashine ya elekroniki. Taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani iliidhinishwa na Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Jean-Pierre Bemba, Moise Katumbi, Freddy Matu...

Waziri Jafo Afunguka Sakata la Mkurugenzi Aliyekamatwa Akitaka Kutoroka Nchi Kuelekea Nchi Jirani

Image
NancyTheDreamtz Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, amesema walimkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’wale, Geita, Carlos Gwamagobe, akitaka kutoroka kwenda nchi jirani baada ya upotevu wa zaidi ya Sh bilioni 2.2. Kauli hiyo aliitoa jijini hapa jana wakati akifunga mafunzo kwa wakuu wa wilaya wapya 27 na wakurugenzi 39 walioteuliwa Julai na Agosti, mwaka huu na Rais Dk. John Magufuli. “Kwa mfano juzi juzi pale Nyang’wale watu wameiba zaidi ya shilingi bilioni 2.2, sio fedha za mchezo eti mfano Halmashauri ya Kakonko inakusanya shilingi milioni 343,” alisema na kuongeza: “Halmashauri nyingine wameiba shilingi bilioni 2.2 sawa na miaka saba ya ukusanyaji wa Kakonko, lakini muda mfupi watu wamechukua akaunti inasoma ziro. “Halafu hawana shaka wanafunga mikanda, nimpongeze mkurugenzi wa Nyang’wale, alionyesha ndani ya muda mfupi anafaa kuwa mkurugenzi. “Alikataa baada ya kuona vitu havijakaa sawa, angeenda kichwa ...