Posts

Kijina wa Sekondari Agundua Simu Isiyotumia Vocha wala Kadi

Image
NancyTheDreamtz Kijana Simon Petrus Mwanafunzi wa Sekondari raia wa Namibia ameuelezea ugunduzi wake kuwa unatumia mawimbi ya redio na hauhitaji kuwa na 'simcard na airtime' - Amesema kuwa imemchukua miaka 2 kukamilisha ugunduzi huo alioufanya kwa kutumia mabaki ya simu na runinga zilizoharibika - Wazazi wake ambao hawana ajira kwa sasa walihangaika kumsaidia kijana wao ili akamilishe mradi huo uliogharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Nne

Mwili wa Mtoto Mdogo Waopolewa Leo Wakati Shughuli ya Kunyanyua Kivuko Ikiendelea...

Image
NancyTheDreamtz Idadi hiyo imefikia baada ya Mwili wa mtoto mmoja kuopolewa leo ambapo shughuli ya kukivuta Kivuko hicho inaendelea Itakumbukwa kuwa jana Septemba 24 miili ya watu wawili iliopolewa katika eneo la ajali hiyo kwenye Ziwa Victoria Aidha, baada ya kufanikiwa kukilaza kwa ubavu Kivuko hicho baadhi ya mizigo ikiwamo mikungu ya ndizi, mikoba na majamvi imeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara Kazi ya kunyanyua kivuko hicho kilichozama Septemba 20 na kujifunika inafanywa na wataalam kutoka JWTZ na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wakishirikiana na Maafisa kutoka kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza

Mizigo ya Waliofariki na Majeruhi Yaanza Kuibuka

Image
NancyTheDreamtz Mizigo zaidi inasukumwa ufukweni kutoka ndani ya kivuko cha Mv Nyerere baada ya wataalam kufanikiwa kukinyanyua na kukilaza ubavu  Ukara. Baadhi ya mizigo ikiwamo mikungu ya ndizi, mikoba na majamvi  iliyokuwa ndani ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozana ziwa Victoroa imeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Hali hiyo imejitokeza baada ya wataalam wa uokoaji kufanikiwa kikilaza ubavu kivuko hicho hicho kilichopinduka Septemba 20 na kujifunika kifudifudi. Kazi ya kunyanyua kivuko hicho inafanywa na wataalam kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wakishirikiana na maofisa kutoka kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza. Operesheni ya uokoaji tayari imefanikisha kuopoa miili ya watu 227 waliokufa katika ajali hiyo, huku wengine 41 wakiokolewa hai.

Esma Azidi Kumkandamiza Mobetto Skendo Ya Uchawi " Tunayajua Mambo Yake Mengi Makubwa Tunalipua Bomu Muda Wowote"

Image
NancyTheDreamtz Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kumtolea povu Hamisa Mobetto na kudai yeye ndio chanzo cha sakata hilo la uchawi kufika mbali. Familia ya Diamond iliingia Kwenye headlines mapema wiki iliyopita baada ya kumtuhumu Mobetto kwa tuhuma za kuwaendea familia yao  kwa mganga. Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum kuhusiana na sakata hilo, Esma alisema amekuwa akizushiwa lawama na matusi kwamba ndiye aliyevujisha ishu hiyo jambo ambalo si kweli. Unajua kama sisi tungekuwa wabaya, basi tungeweka kila kitu kwenye mitandao, lakini kutokana na watu hawaelewi, wanatutukana na kutusema vibaya kwa sababu tu hawajui ukweli wa hili jambo”. Esma alizidi kutiririka na kudai kuwa anawashangaa watu kuwaona wao kama wakosefu na labda hawampendi Hamisa, lakini siyo kweli ni kwa sababu tu mwanamitindo huyo anatengeneza sura ya huruma kwa watu. Watu wanaweza kusema mama yangu ana matatizo, lakini siyo, kwa sababu h...

Huyu Ndie Mchungaji Aliyepigwa Risasi 40 na Majambazi Bila Kupenya Mwilini

Image
NancyTheDreamtz Wakati ulimwengu ukibuni njia ya kuweza kubuni mavazi ambayo yatazuia risasi kutokupenya kiurahisi kwenye mwili wa binadamu, hii ni tofauti kwa Mchungaji wa Kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry International, David Elijah kutoka Nigeria ambaye wiki iliyopita amenusurika kifo kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani. Mchungaji David siku ya Ijumaa Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria alikuwa anaenda kanisani kwake akiwa kwenye gari alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi. Gari hilo lilitobolewa karibia lote kwa risasi lakini mpaka maaskari wanafika eneo la tukio, walimkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo. Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo. Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji huyo s...

John Makini Awajia Juu Wanaom’beza Mdogo WakeNiya Yake ya Urais

Image
NancyTheDreamtz Kaka wa rapper Nikki wa pili wa kundi la Weusi, Joh Makini amewajia juu wanaomponda na kum’beza mdogo wake, kutokana na uamuzi wa kutangaza nia na ndoto yake ya kuwa Rais. ‘’Ni kitu kizuri kwa mtu kuwa na ndoto kubwa na kitu kilichonisikitisha pale tu Nikki Wa Pili alitangaza ndoto yake kubwa ya kuwa Rais wa Tanzania alikutana na vipingamizi vikubwa kwa watu wengi wakiona kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani inaonyesha ni jinsi gani tuko katika taifa la watu wasio na ndoto, ni kitu kibaya sana lazima uwe na ndoto, lazima uwe na kitu kinachokwambia kwamba siku moja wewe utakuwa mtu fulani na ukiifanyia kazi hiyo ndoto yako utaweza kuifanikisha maana hapa chini ya jua hakuna kinachoshindikana, kwahiyo namtakia kila la heri na baraka zote atimize ndoto zake’’ Alisema John Makini akifanya mahojiano na mtandao wa www.cloudsfm.co.tz

Picha ya Irene Uwoya Yazua Balaa Mtandaoni

Image
NancyTheDreamtz BigieMsanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya amejikuta akiibua mjadala mkubwa mara baada ya kuachia picha ambayo inaonyesha eneo la kifuani likiwa wazi kwa asilimia kubwa. Mremmbo huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuweka picha hiyo ambapo mashabiki wake wamejikuta wakichagia kwa wingi kuliko ilivyo kawaida kuhusu picha hiyo  Picha iliyozua gumzo