John Makini Awajia Juu Wanaom’beza Mdogo WakeNiya Yake ya Urais

NancyTheDreamtz
John Makini awajia juu wanaom’beza mdogo wake, kisa Urais
Kaka wa rapper Nikki wa pili wa kundi la Weusi, Joh Makini amewajia juu wanaomponda na kum’beza mdogo wake, kutokana na uamuzi wa kutangaza nia na ndoto yake ya kuwa Rais.



‘’Ni kitu kizuri kwa mtu kuwa na ndoto kubwa na kitu kilichonisikitisha pale tu Nikki Wa Pili alitangaza ndoto yake kubwa ya kuwa Rais wa Tanzania alikutana na vipingamizi vikubwa kwa watu wengi wakiona kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani inaonyesha ni jinsi gani tuko katika taifa la watu wasio na ndoto, ni kitu kibaya sana lazima uwe na ndoto, lazima uwe na kitu kinachokwambia kwamba siku moja wewe utakuwa mtu fulani na ukiifanyia kazi hiyo ndoto yako utaweza kuifanikisha maana hapa chini ya jua hakuna kinachoshindikana, kwahiyo namtakia kila la heri na baraka zote atimize ndoto zake’’ Alisema John Makini akifanya mahojiano na mtandao wa www.cloudsfm.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele