Esma Azidi Kumkandamiza Mobetto Skendo Ya Uchawi " Tunayajua Mambo Yake Mengi Makubwa Tunalipua Bomu Muda Wowote"

NancyTheDreamtz
Esma Azidi Kumkandamiza Mobetto Skendo Ya Uchawi " Tunayajua Mambo Yake Mengi Makubwa Tunalipua Bomu Muda Wowote"
Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kumtolea povu Hamisa Mobetto na kudai yeye ndio chanzo cha sakata hilo la uchawi kufika mbali.

Familia ya Diamond iliingia Kwenye headlines mapema wiki iliyopita baada ya kumtuhumu Mobetto kwa tuhuma za kuwaendea familia yao  kwa mganga.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum kuhusiana na sakata hilo, Esma alisema amekuwa akizushiwa lawama na matusi kwamba ndiye aliyevujisha ishu hiyo jambo ambalo si kweli.

Unajua kama sisi tungekuwa wabaya, basi tungeweka kila kitu kwenye mitandao, lakini kutokana na watu hawaelewi, wanatutukana na kutusema vibaya kwa sababu tu hawajui ukweli wa hili jambo”.

Esma alizidi kutiririka na kudai kuwa anawashangaa watu kuwaona wao kama wakosefu na labda hawampendi Hamisa, lakini siyo kweli ni kwa sababu tu mwanamitindo huyo anatengeneza sura ya huruma kwa watu.

Watu wanaweza kusema mama yangu ana matatizo, lakini siyo, kwa sababu hata huyo mganga hakuwa anamjua, bali ni ndugu wa huyo mganga ndiye anafahamiana na mama na kwa vile aliona ni watu ambao wanakuwa pamoja kwenye vitu mbalimbali ndiyo akamwambia huyo ndugu yake na mama akayapata.

Najua kabisa ukweli wao wanafahamu, lakini wanapenda kupindisha mambo na hayo yaliyosikika ni madogo mno, yapo mengine na tuna ushahidi wa kutosha hivyo na sisi tukiamua tutalipua bomu muda wowote“.

Baada ya sakata hilo kutokea watu kadhaa waliibuka na kumkingia kifua Hamisa na kuilaumu familia ya Diamond kwa kitendo kile walichomfanyia mama Watoto wa Diamond.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele