Posts

Showing posts from January, 2020

Waziri Lugola Awaondoa Madarakani Maafisa Wa NIDA Mkoa Wa Ruvuma

Image
NancyTheDreamtz Na Mwandishi Wetu, MOHA, Songea. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola  amemuondoa madarakani Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Ruvuma, Seif Mgonja kwa kosa la kutogawa kwa wananchi Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN), 14,493 tangu Disemba 31, 2019, licha ya kuzalishwa na Makao Makuu na kuletewa ofisini kwake Mjini Songea. Pia Waziri Lugola amemuondoa madarakani Afisa wa NIDA Wilaya ya Namtumbo, Mkoani humo, Thobias Nangalaba kwa uzembe wa kutofika katika kikao chake cha viongozi wa Mkoa na Wilaya, licha ya kupewa taarifa ya kuhudhuria kikao hicho. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Soko Kuu la Manispaa ya Songea Mkoani humo, leo, Waziri Lugola amesema, amewatengua vyeo maafisa wawili hao kwa kucheza na kazi za Serikali, kwa kutojali majukumu yao. “Ndugu wananchi wa Songea, maafisa hawa wamekuwa wakienda kinyume na maagizo ya Serikali la kuwataka waweze kuwakamilishia wananc...

Waziri Mabula Aitaka Bodi Ya NHC Kupitia Upya Gharama Za Nyumba Inazouza

Image
NancyTheDreamtz Na Munir Shemweta, WANMM MASASI Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia upya gharama za nyumba zake ilizojenga maeneo ya pembezoni kwa ajili ya kuziuza. Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana wilayani Masasi mkoa wa Mtwara wakati alipotembelea mradi wa nyumba 54 zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Kusini pamoja na kutembelea miradi inayofanywa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Kauli hiyo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia kulalamikiwa na wabunge wa Majimbo ya Masasi Dkt Rashid Chuachua na yule wa jimbo la Lulindi  mkoani Mtwara Jerome Bwanausi kuwa pamoja na halmashauri kuhitaji nyumba kwa ajili ya watumishi lakini gharama imekuwa kubwa kiasi cha halmashauri na wananchi kushindwa kuzinunua. ‘’ Ni vizuri bodi ikae iangalia namn...

Breaking: Matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Pili Yametoka....Bofya Hapa

Image
NancyTheDreamtz Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Alhamisi, Januari 9, 2020 limetangaza matokeo ya mtihani wa upimaji darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne. Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema ufaulu katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne umeongezeka kwa asilimia 26.21. Jumla ya watahiniwa 1,531,120 kati ya wanafunzi 1,665, 863 wamepata alama A,B,C na D ikilinganishwa na wanafunzi 1,213, 132 waliofaulu mwaka 2018. Katika mtihani wa upimaji kidato cha pili, wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya wanafunzi 571,137 wamefanya vizuri katika mtihani huo na kuwawezesha kuingia kidato cha tatu. Dk Msonde amesema mtihani wa kidato cha nne jumla ya watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722 wameefaulu mitihani yao. Watahiniwa hao ni sawa na ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na watahiniwa 284,126 sawa na asilimia 79.27 waliofaulu mtihani huo mwaka 2018.

Daimond: Nimeenda kwenye tuzo nyingi sana ila tuzo za CAF ni ya kipekee

Image
NancyTheDreamtz Msanii Daimond platinum amerejea nchini na kufunguka show yake aliyoifanya katika tuzo za CAF ambazo zilifanyika nchini misri ikiwa kwake ni mara ya pili na kusema kuwa ilikuwa nzuri kwakuwa waandaaji walijipanga. Akifanyiwa mahojiano na wasafi media amesema kuwa yeye ndo msanii pekee toka Afrika ambaye alipata nafasi za kualikwa na kufanya show katika tuzo hizo na kusema kuwa  kati ya show zake zote hii ndo alilipwa vizuri. ''Kiukweli Nimefanya Show Nyingi na Malipo ya Show Hii ya CAF Nililipwa Vizuri sio Uongo na nimehudhuria Tuzo nyingi sana Duniani, lakini tuzo za CAF Kiukweli Jamaa Walijipanga sanaaaaa kwasababu walikuwa na maandalizi ya Hali ya juu'' alisema Daimond.

Mrembo Huddah MonroeAkana Kumpa UTAMU Harmonize

Image
NancyTheDreamtz DAR: Siyo taipu yangu! Sosholaiti ambaye ni modo maarufu nchini Kenya ameibuka na kukana kumpa penzi staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ akidai eti siyo taipu yake. Huddah ambaye ni shoga wa mzazi mwenza wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka hayo baada ya kupita muda mrefu tangu alipodaiwa kutembea na Harmonize au Harmo miaka kadhaa iliyopita. Kupitia vyombo vya habari vya Kenya hivi karibuni, Huddah ameapa kuwa hajawahi kumvulia nguo ya ndani jamaa huyo kama wengi wanavyoamini. Huddah amefunguka kuwa, video iliyosambaa miaka miwili iliyopita ikimuonesha akiwa kimahaba na Harmo ilikuwa nchini Afrika Kusini wakila bata. Alisema kuwa, siku hiyo alikuwa na Zari ambaye wakati huo alikuwa mpenzi wa Diamond au Mondi ambapo walikuwa wamekaa pamoja ndipo wakajirekodi kipande hicho cha video na baada ya hapo kila mmoja aliendelea na hamsini zake. Alisisiti...

Rasmi Mbwana Samatta Aaga Genk na Kutimkia Uingereza

Image
NancyTheDreamtz MSHAMBULIAJI wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mtanzania, Mbwana Samatta amewaaga wachezaji na viongozi wa timu hiyo tayari kwa safari yake kwenda kucheza Ligi Kuu England ‘Premier League’.   Samatta anatajwa kuwaniwa na Norwich City inayoshiriki katika Premier ikidaiwa kuwa imeweka mezani dau la pauni milioni 11 (Sh bilioni 33).   “Samatta sasa hivi hayupo Ubelgiji ameshaaga wachezaji, viongozi na mashabiki juu ya suala la usajili wake wa kwenda kucheza England kwa sababu klabu zinazohitaji huduma yake ni nyingi. “Unajua alitakiwa aondoke muda sana isipokuwa wakala wake wa awali alikuwa akimsubirisha na muda unapotea, baadaye ndipo akabadili wakala, ambapo tayari kuna ofa ya hao Norwich, pia kuna West Ham na Brighton ni jambo la kusubiria kuona itakuaje,” alisema mzee Samatta.  

Makubwa..Wazazi Wamuua Mwalimu kwa Moto KISA Matokeo

Image
NancyTheDreamtz Imeelezwa kuwa mnamo Januari 6, 2020, nchini Kenya, wazazi walimshambulia mwalimu kwa moto hadi kupelekea umauti kwa madai kwamba wanalalamikia matokeo mabaya ya mtihani wa Darasa la nne. Tume ya kuajiri walimu nchini Kenya (TSC), kupitia kwa Mkurugenzi wake, Nancy Macharia, imelaani kitendo cha baadhi ya wazazi hao kumshambulia na kumchoma moto mwalimu, Daisy Mbathe Mbaluka wa shule ya msingi Ndooni nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Januari 9 mwaka huu na Tume hiyo, imeamuru walimu Sita waliopo katika shule hiyo, kuondoka mara moja na kwamba haitoweza kupeleka tena walimu shuleni hapo hadi pale itakapohakikishiwa usalama wao kwanza. Aidha taarifa zinaeleza kuwa tayari watu wawili wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho wamekwishakamtwa.

TID Afunguka Kuhusu Taarifa Zinazosemekana Kuwa WASANII Walioenda Kigoma Kumsapoti Dimaond Hawajalipwa – Video

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa Bongo Fleva @tidmusic Mnyama amefunguka kuhusu maneno yaliyokuwa yanasambaa kuwa wasanii wote waliomsindikiza Diamond kwenda Kigoma hawakulipwa. Mbali na hilo TID sameeleza mipango yake kwamba anataka kufanya Annivensary ya miaka 19 kwenye muziki wake kama alivyofanya @diamondplatnumz Kigoma lakini yeye ataifanyia Dar Es salaam sehemu alipozaliwa, Pia amezungumzia kipaji cha msanii chipukizi wa Kike ambaye ni mtoto wa Mtangazaji wa Clouds Fm Gadna @malkiakaren na kusema atafika mbali sana kwani ana kipaji cha kipekee sana.

Simba SC Waifuata Mtibwa SUGAR Fainali Mapinduzi Cup 2020

Image
NancyTheDreamtz Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo walicheza mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2020 dhidi ya Bingwa mtetezi Azam FC katika uwanja wa Amaan, Simba SC ambao walikuwa na kumbukumbu mbaya dhidi ya Azam katika michuano hiyo baada ya mwaka jana kupoteza dhidi ya Azam FC hatua ya fainali. Safari hii imeonekana wamekuja kitofauti na kuwa makini zaidi licha ya timu yao kukosa nafasi kadhaa za wazi wakati wa mchezo, dakika 90 ziliisha bila timu yoyote kupata matokeo chanya (0-0), ndipo muamuzi alipoamua kuitisha mikwaju ya penati kama sheria za mashindano hayo zinavyosema na kumalizika kwa Simba SC kushinda kwa penati 4-2. Matokeo hayo ni wazi Simba SC katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo atacheza January 13 2020 dhidi ya Mtibwa Sugar ambao jana, walifuzu kucheza fainali kwa kumfunga Yanga SC kwa penati 4-2, hiyo ni baada ya mchezo huo dakika 90 kuisha 1-1