Chama Aongeza Mkataba Mpya Simba SC
NancyTheDreamtz MFUNGAJI wa mabao ya mwisho yaliyoipeleka hatua ya makundi na Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika timu ya Simba Mzambia, Clatous Chota Chama ‘Triple C’ ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea timu hiyo. Huyo, ni mchezaji wa sita kwa Simba kuongezewa mkataba wengine ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Aishi Manula, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Meddie Kagere. Chama alijiunga na Simba kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akitokea Power Dynamo inayocheza ligi ya nchini huko. Taarifa ya klabu ya Simba inaeleza kuwa kiungo huyo atakuwa sehemu ya kikosi hicho hadi 2020 baada ya kuongeza mkataba huo. Simba hivi sasa ipo kwenye mikakati ya kukiboresha kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kimataifa Afrika na kikubwa kufika hatua ya fainali baada ya msimu uliopita kufika robo fainali. Timu hiyo hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kuwasajili wachezaji wapya watano ambao ni Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Gerson Fraga ...