Vurugu Hotelini… Ebitoke Amponza Mlela! we
NancyTheDreamtz KIKI imemtokea puani! Komediani na mwigizaji maarufu wa kike wa filamu za Kibongo asiyeishiwa vituko, Annastazia Exavery almaarufu kama Ebitoke, amempoza mwigizaji Yusuf Mlela, Amani limedokezwa. Jumatatu ya Novemba 11, mwaka huu, Ebitoke alivamia mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Mlela kwenye Hoteli ya Protea jijini Dar na kufanya vurugu zilizozua gumzo kila kona. TUKIO LA KUTENGENEZA (KIKI) Katika tukio hilo ambalo ni la kutengeneza (kiki) kwa asilimia mia moja, Ebitoke alifika mahali hapo na kwenda kumvua wigi mrembo aliyesemekana anatoka na Mlela aliyetajwa kwa jina la Beyonce na kumwacha akiwa na kipilipili kichwani, lakini lawama zote sasa zinaelekezwa kwa Mlela huku kukiwa na shinikizo la kuchukuliwa hatua. EBITOKE ALIA KUSALITIWA Kabla ya tukio hilo, siku chache zilizopita Ebitoke alilia mbele ya gazeti hili akilalamika kusalitiwa kimapenzi na kuchezewa na Mlela baada ya jamaa huyo kunaswa na Beyonce kwenye birthday ya mwigizaji Aunt Ezekie...