Ruby Yamfika Hapa! Atoboa Mazito Anayoyapitia kutoka kwa Mzazi Mwenie "Nimepata Vipigo, Manyanyaso na Fedhea"

NancyTheDreamtz

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwenye ukurasa wa msanii Ruby, ameweka wazi visa ambavyo anafanyiwa na mpenzi wake aitwaye Kusah, kwa kupigwa,  kunyanyaswa, kudhalilishwa na kupewa kashfa za kujihusisha kwenye mahusiano na wasanii wa kiume.


Hali inaashiria kwa sasa wawili hao wameachana na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike, ila Ruby aliandika kuwa yeye sio muongeaji sana wa mambo ila leo acha aongee.

"Nimekuwa nikijiuliza niseme ama niongee kwa nani, huenda nayopitia au niliomaliza kupitia yanampata binti  wa kike mwenye umri kama wangu au zaidi yangu ila tu amekuwa kifungoni, Nimepitia vipigo, manyanyaso, fedhea, kudhalilishwa na kuitwa majina yote kutoka katika kinywa na mikono ya Mwanaume ambae alikuja kwangu kutaka support" ameandika Ruby.

"Nimejitahidi kwa uwezo wangu kukuunganisha na kaka yangu, mwisho wa siku unishushie makofi natembea nae, ukuishia apo unayasambaza na ya mtu tunayeheshimiana Juma Jux kusema natembea naye, hii kama mtoto wa kike inaniharibia taswira mbele ya jamii yangu" ameongeza.

Pia Ruby ameitaka Serikali ya Tanzania kuimarisha adhabu dhidi ya wanaume wanaowafanyia wasichana na wanawake vitendo kama hivyo sio kuishia mahakamani tu na kulipa faini ya shilingi 50,000 au kifungo cha miezi 6.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele