Utabiri wa Bongozozo mechi ya Stars,ataja mfungaji

NancyTheDreamtz

Shabiki wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' aliyejizolea umaarufu hivi sasa hapa nchini, Nicky, maarufu kama 'Bongozozo' ametoa utabiri wake kuelekea mchezo wa leo wa Taifa Stars dhidi ya Equitorial Guinea pamoja na mfungaji.


Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa taifa, ikiwa ni kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2021 nchini Cameroon.

Akizungumza na EATV & Radio Digital, Bongozozo amesema kuwa angependa Stars ishinde mabao manne au hata sita ili afurahi na kumtaja mshambuliaji Farid Mussa kuwa ndiye atakuwa mfungaji wa leo kwenye mchezo huo.

"Ni muhimu sana uende uwanjani au usikilize na ufurahie mpira, ni kama sherehe fulani. Leo tutashinda magoli mengi tena itakuwa bila, inaweza kuwa tatu bila, mbili bila au ingekuwa sita bila ingekuwa balaa, lakini ninavyotabiri itakuwa mbili bila kwakuwa Kaseja hapitiki pale.", amesema Bongozozo.

"Farid Mussa anafunga leo, nilienda kuonana naye nikampa ngucu za Bongozozo ili awe na nguvu na uchangamfu wa kufunga.", ameongeza.

Mchezo huo unatarajia kupigwa saa 1:00 usiku wa leo, na kauli mbiu ya kila mtanzania kuelekea mchezo huo ikiwa ni 'TwenzetuTena'.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele