Diamond, Rayvanny Waiomba Msamaha BASATA na Serikali .....Waahidi Kutorudia Makosa
NancyTheDreamtz
Mwanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny wameomba radhi kwa kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), huku wakiwasihi wasanii wenzao kuwa mabalozi wazuri wa utamaduni wa Tanzania.
“Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi Serikali, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Basata na kila aliyekwazika tulivyoimba wimbo wa Mwanza katika Wasafi Festival mkoani Mwanza,” amesema Diamond.
Wanamuziki hao wameomba radhi baada ya Basata kutangaza kuwafungia kwa muda usiojulikana likidai kufikia uamuzi huo baada ya wasanii hao Jumamosi Desemba 15, 2018 kuonyesha dharau kwa kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na baraza hilo.
Mbali na kuwafungia wanamuziki hao, Basata imetangaza kukifuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival.
Video inayosambaa mtandaoni leo Ijumaa Desemba 21, 2018 inamuonyesha Diamond akiwa pamoja na Rayvanny, kwa pamoja wakiomba radhi mamlaka husika.
“Japo tunajitahidi kuwa vijana wenye mfano bora kwa Taifa letu lakini kama ujuavyo binadamu siku zote hatuwezi kupatia hutokea tukakosea, na kweli tumekosea kuimba wimbo ambao umefungiwa,” amesema Diamond.
“Tunaahidi kutorudia tena kwa kosa lililotokea lakini pia kupitia kazi zetu za sanaa kuwasihi mashabiki na wasanii wenzetu kuwa mabalozi wazuri kwa tamaduni zetu za Tanzania
Comments