Bao Alilofunga Ndemla Jana Dhidi ya KMC Lazua Gumzo

NancyTheDreamtz
Bao Alilofunga Ndemla Jana Dhidi ya KMC Lazua Gumzo
Shuti alilopiga kiungo wa Simba, Said Hamis Ndemla dakika ya 14 akimalizia pasi ya Mzamiru Yasin na kumshinda mlinda mlango wa KMC Jonathan Nahima, limekuwa gumzo kubwa.

Simba ilishinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Shuti hilo la Ndemla akitumia mguu wa kulia nje ya 18 limekuwa gumzo kubwa mitandaoni.

Ndemla alipiga shuti hilo haraka sana baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mzamiru na kuwaduwaza KMC.

Mjadala huo umekuwa ukiendelea namna shuti hilo alivyoweza kulipiga haraka na kuweza kulenga lango.


Ndemla amekuwa akikaa benchi kutokana na Simba kuwa na kikosi kipana lakini jana alikuwa mmoja wa wachezaji walioonyesha wanaweza kufanya vema wakipata nafasi.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele