Samatta na Msuva waiangamiza Cape Verde Uwanja wa Taifa

NancyTheDreamtz
Washambuliaji wawili wanaochezea soka la nje Mbwana Ally Samatta na Saimon Msuva wamefanikiwa kuitoa kimasomaso timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kuisaidia kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wapinzani wao Cape Verde. Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza ambao ulifanyika Cape Verde Taifa Stars walipoteza kwa kufungwa jumla ya goli 3-0.
Magoli ya leo yamepatikana dakika ya 28 goli lililofungwa na Saimon Msuva baada ya kupokea mpira kutoka kwa Samatta,hadi mapumziko timu hizo zilienda kwa Stars kuongoza kwa goli moja licha ya Samatta kukosa mkwaju wa penati mnamo dakika ya 23 ya mchezo.
Kipindi cha pili kilipoanza Stars walijipatia goli la pili mnamo dakika ya 58 lililofungwa na mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Ally Samatta baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mdathiri Yahya na Samatta kufanikiwa kumalizia goli hilo kwa shuti kali.
Lakini mnamo dakika ya 89 taa za Uwanja wa Taifa zilizima na mashabiki kuwasha taa za simu zao kuonyesha ni jinsi gani wamefurahishwa na matokeo hayo.
Kwa matokeo hay sasa Stars wanakuwa katika nafasi ya pili wakiwa na alama 5 nyuma ya kinara Uganda mwenye alama 7 huku Cape Verde wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 4 na Lesotho wakishikilia mkia kwa alama 2 huku mchezo wao dhidi ya Uganda ukiwa bado haujachezwa.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele