Irene Uwoya afunguka kuhusiana na ndoa yake na Dogo Janja “Alishawahi kuchepuka kwenye ndoa”

NancyTheDreamtz
Msanii muigizaji kutoka katika tasnia ya Bongo Movie Irene Uwoya amefunguka mwanzao mwisho kuhusiana na maisha yake lakini pia kuhusiana na maisha ya ndoa ambayo alioana na msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja.
Msanii huyo ameongea hayo wakati anapiga stori katika kipindi cha PlayList kinachofanyika katika kituo cha habari cha TimesFm, Irene amefunguka kuhusiana na maisha yake lakini haswa kuhusiana na yale yanayoendelea kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ile kinachosemekana ameachana na mume wake huyo ambaye ni Dogo Janja.
Irene amesema kuwa ” Yeye kuonekana yuko nje ya nchi akionekana anakula bata bila Dogo Janja,Kila mtu anazungumza kile anachohisi kuzungumza na mimi siwezagi kuongelea mambo yangu kwenye media, Mimi kuonekana nje niko kwenye biashara zangu mbona Dogo Janja akiendaga kufanya video za nyimbo zake mfano Afrika ya Kusini hanibebagi ? kwahiyo mimi naendaga kibiashara kama yeye anavyoendaga kikazi. lakini katika ndoa yake haoni kama kuna tatizo kwani kila kitu kipo sawa kuhusiana na yeye na Dogo Janja”
Lakini ilipofika muda wa maswali ya “Ndio au Hapana” kuna maswali ambayo Irene alikataa kuyajibu yanayomuhusu Dogo Janja na kumwambia Lil Ommy uliza swali lingine,Maswali yalikuwa hivi:-
Swali la kwanza – Ni kweli mmeachana na Dogo Janja ?….. Irene alikataa kulijibu na kusema uliza swali lingine,
Swali la pili – Ni kweli hamkai pamoja na Dogo Janja ?…….Irene alikataa pia kulijibu na kusema uliza lingine
Swali la tatu – Ni kweli Umemu-Uniffolow Dogo Janja Instagram …? Irene alijibu “Hapana”
Swali la tatu – Ni kweli mnategemea mtoto na Dogo Janja….. Irene alikataa kulijibu na kusema Swali lingine
Swali la nne – Ni kweli Dogo Janja alishawahi kuchepuka kwenye ndoa yenu ?….Irene alijibu “Ndio”
Swali la tano – Ni kweli Irene Uwoya alishawahi kuchepuka kwenye ndoa yake ?…… Irene alijibu “Hapana”
Lakini baada ya kumaliza maswali yote aliulizwa kwanini katika nyimbo zote alizozichagua hakuchagua nyimbo yoyote ya Dogo Janja na kusema “Mimi nilijua tunachagua nyimbo za wasanii wa nje tu” Irene Uwoya hakuishia hapo aliwakaribisha Watanzania wote katika Night Club yake anayotarajia kuifungua muda sio mrefu maeneo ya Sinza ambayo itaitwa “Last Minutes”

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele