Posts

Showing posts from 2018

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Rais Magufuli Kuamuru Kikokotoo cha Zamani Kitumike Mafao ya Wastaafu

Image
NancyTheDreamtz Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe  amempongeza Rais John Magufuli kwa kukubali ushauri walioutoa na kuacha upande wa waziri, washauri wake na watendaji wa Serikali yake. Maoni ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameyatoa leo baada ya Rais Magufuli kurejesha utaratibu wa awali wa kikokotoo cha asilimia 50 kwa watumishi wa Serikali na asilimia 25 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. “Kufuatia uamuzi wa Rais Magufuli kuhusu kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa wastaafu , sisi ACT Wazalendo na vyama vya upinzani kwa ujumla tumesimama na wafanyakazi toka mwanzo wa sakata hili, wakati sheria ikiwa muswada na hata baada ya kanuni kutungwa,” amesema  “Kwetu, jambo lolote linaloongeza maslahi na ustawi wa wafanyakazi ni jambo jema na muhimu. Tunashukuru kuwa Mheshimiwa Rais ametuelewa na amekuja upande wetu na na kuacha upande wa waziri wake, washauri wake na watendaji wa Serikali yake,” ameongeza.  “Tunapoelekea mbele, tunamuomba a...

Serikali Yazifunga akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa Korosho Kupisha Uhakiki

Image
NancyTheDreamtz Serikali imefunga kwa muda akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa korosho kupisha uhakiki wa kina wa umiliki wa korosho walizouza. Uamuzi huo unakuja wakati ikiwa imeshaingiza Sh3.8 bilioni kwenye akaunti hizo katika mfululizo wa uhakiki na ulipaji wakulima wa zao hilo unaoendelea nchini. Akizungunza na gazeti la The Citizen, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wakulima wenye akaunti hizo wameuza zaidi ya kilo 1,500 kwenye vyama tofauti vya msingi, hivyo ni lazima umiliki wa korosho walizouza uhakikiwe. “Hatua hii ni muhimu (ya kufunga akaunti hizi kwa muda) ili kupisha uhakiki kwa sababu utaratibu unataka mkulima aliyeuza zaidi ya kilo 1,500 za korosho aonyeshe shamba lake lilipo kwa timu yetu ya uhakiki,” alisema Hasunga “Lakini uchunguzi wa awali umeonyesha kuna baadhi ya wakulima wameuza kiasi kinachofikia kilo 3,000 za korosho kwenye vyama vya msingi tofauti.” Hata hivyo, waziri huyo alisema Serikali bado haijapata kiasi ha...

Walichokisema Sumaye, Zitto Kabwe Baada ya Tundu Lissu Kusema Yupo Tayari Kugombea Urais 2020

Image
NancyTheDreamtz Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema wanamsubiri kwa hamu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu apitishwe na chama chake kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020. Lissu anayetibiwa nchini Ubelgiji baada ya shambulio la risasi zaidi ya 30 lililotokea Septemba 7, mwaka jana akiwa Dodoma, juzi aliliambia gazeti la Mwananchi kwamba hatakuwa na kipingamizi ikiwa chama chake kitampitisha kuwania nafasi hiyo. Kauli ya Lissu ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya CCM, imepokewa kwa furaha na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiamini anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa chama tawala. Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe alisema Lissu atavifaa vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020. Maoni ya Rungwe yaliungwa mkono na Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alisema hana shida na kauli ya Lissu. “Jambo la muhimu kuliko yote ni kuwa mwaka 2019, kwetu ni mwaka wa kudai demokrasia. Azimio la Zanzibar limeweka mpango ma...

Kwa Hili la Mwanamuziki Diamond, Basata Mnajitukanisha Wenyewe

Image
NancyTheDreamtz BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) chini ya katibu mkuu wake, Godfrey Mngereza, ni kama limepoteza mwelekeo. Viongozi wake wamekuwa na ndimi mbilimbili, maamuzi yao hayana nguvu tena na hata umuhimu wake wa kuwepo, haupo. Ukitazama sarakasi zinazoendelea kati ya Basata na wasanii Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) na Raymond Mwakyusa (Rayvanny), kuhusu kufungiwa kwa wimbo wa Mwanza (Nyegezi), unaweza kuwafananisha Basata na mbwa mkubwa asiye na meno, anaishia kubweka tu lakini hawezi kung’ata.  Novemba 12, 2018 (mwezi uliopita), Basata walitangaza kuufungia wimbo wa Mwanza (Nyegezi) wa Rayvann na Diamond Platnumz. Wakati Basata wakitangaza kuufungia wimbo huo kwa sababu za kimaadili, hatua hiyo ilikuwa imekuja kwa kuchelewa.  Unafungiaje wimbo ambao tayari watu wameshaudownload, watu wanao kwenye simu zao, kwenye laptop zao, kwenye vyombo vyao vya usafiri mpaka majumbani mwao? Licha ya kutangaza kuufungia wimbo huo, na kuwakataza wasanii husika kutoupiga sehemu...

Waziri Jafo Abaini UFISADI Wa Mabilioni Ulanga

Image
NancyTheDreamtz OFISI ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) imebaini matumizi mabaya ya fedha za serikali Sh. bilioni 2.98 katika halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wakuu wa idara wote waliohusika wavuliwe nyadhifa zao huku watumishi wengine waondolewe majukumu ili vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria dhidi yao. Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Twala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uchunguzi maalum uliofanywa kwa halmashauri ya wilaya hiyo. Jafo alisema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imefanya uchunguzi maalum katika halmashari 12 nchini ambazo ni Ulanga, Same, Mbulu, Meru, Itigi, Misungwi, Nyang’hwale, Serengeti, Bahi, mpwapwa, Morogoro Dc na Kibaha Tc ambapo katika halamasahuri ya Ulanga uchuguzi ulianza Novemba 13 hadi 23 mwaka huu. Alisema uchunguzi huo ulifanyika kufuatia malalamiko ya wanachi mbalimbali pamoja na mbunge wa jimbo la Ulang...

Q-chiller Azimika na Sauti ya Isha Mashauzi.

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa siku nyingi Q-chiller amefunguka na kusema kuwa kila msanii amekuwa na sauti yake na radha yake ya muziki kwa upande wake anaona kuwa moja ya sauti za wasanii zinazomkonga nyoyo ni  sauti ya mwanadada muimbaji Isha Mashauzi. Isha mashauzi ni moja ya wasanii wa kike walioo katika game kwa muda mrefu na wameweza kulinda heshima ya muziki wa taarabu kutokana na sauti yake lakini pia kuipenda kazi yake ya muziki. Q-Chiller amekuwa moja ya wasanii wanaosema wazi sana kuhusu vile wasanii wnegine wamekuwa wakifanya kazi na mafanikio yao pia.

Diamond na mpenzi wake Watinga na Balozi wa Tanzania nchini Comoro

Image
NancyTheDreamtz    Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amekutana na balozi wa Tanzania nchini Comoro.  Katika hafla hiyo Diamond alikuwa ameongozana na mpenzi wake kutoka nchini Kenya, Tanasha. "Earlier today when i visited the Tanzanian Embassy in Comoros," ameandika Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Slide Pointer Device

Image
NancyTheDreamtz  This how Technology Changes in Computer Revolution (User)

CHADEMA Kulipa Fidia Wananchi Waliobomolewa Nyumba zao

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) amewataka wananchi wa Ubungo kuhifadhi vyema nyaraka zao za maeneo waliyobomolewa na kwamba CHADEMA ikiingia madarakani watahakikisha wanawalipa fidia zao.   Kubenea ameyasema hayo jana  ikiwa ni siku moja kupita tangu Rais John Pombe Magufuli alipotamka hadharani kuwa wahanga waliobomolewa nyumba kuanzia maeneo ya Ubungo hawatalipwa fidia kwa kuwa walivunja sheria kwa kujenga kwenye hifadhi ya barabara. Akizungumza jana na wanahabari, Kubenea amedai kushangazwa na kauli ya rais kwamba waliovunjiwa nyumba walijenga kwenye hifadhi ya barabara lakini serikali ndiyo iliyokuwa ikipokea kodi zao, kuwapatia hati za maeneo, kuwawekea maji na umeme huku wakijua hilo ni eneo la hifadhi. "Naomba wananchi wa Ubungo, Kimara waliovunjiwa nyumba zao wahifadhi vizuri nyaraka zao. Mungu akipenda Sisi CHADEMA tukiingia madarakani tutalipa waathirika wote waliobomolewa kuanzia ubungo hadi Kibaha. Inawezekana siyo...

Diamond, Rayvanny Waiomba Msamaha BASATA na Serikali .....Waahidi Kutorudia Makosa

Image
NancyTheDreamtz Mwanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny wameomba radhi kwa kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), huku wakiwasihi wasanii wenzao kuwa mabalozi wazuri wa utamaduni wa Tanzania. “Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi Serikali, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Basata na kila aliyekwazika tulivyoimba wimbo wa Mwanza katika Wasafi Festival mkoani Mwanza,” amesema Diamond. Wanamuziki hao wameomba radhi baada ya Basata kutangaza kuwafungia kwa muda usiojulikana likidai kufikia uamuzi huo baada ya wasanii hao Jumamosi Desemba 15, 2018 kuonyesha dharau kwa kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na baraza hilo. Mbali na kuwafungia wanamuziki hao, Basata imetangaza kukifuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival. Video inayosambaa mtandaoni leo Ijumaa Desemba 21, 2018 inamuonyesha Diamond akiwa pamoja na Rayvanny, kwa pamoja wakiomba radhi mamlaka husika. “Japo tunajitahidi kuwa vijana wenye mfano bora kwa Taifa ...

Bao Alilofunga Ndemla Jana Dhidi ya KMC Lazua Gumzo

Image
NancyTheDreamtz Shuti alilopiga kiungo wa Simba, Said Hamis Ndemla dakika ya 14 akimalizia pasi ya Mzamiru Yasin na kumshinda mlinda mlango wa KMC Jonathan Nahima, limekuwa gumzo kubwa. Simba ilishinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Shuti hilo la Ndemla akitumia mguu wa kulia nje ya 18 limekuwa gumzo kubwa mitandaoni. Ndemla alipiga shuti hilo haraka sana baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mzamiru na kuwaduwaza KMC. Mjadala huo umekuwa ukiendelea namna shuti hilo alivyoweza kulipiga haraka na kuweza kulenga lango. Ndemla amekuwa akikaa benchi kutokana na Simba kuwa na kikosi kipana lakini jana alikuwa mmoja wa wachezaji walioonyesha wanaweza kufanya vema wakipata nafasi.

Paul Pogba Aonyesha Furaha Yake Muda Mchache Baada ya Mourinho Kutimuliwa Man U

Image
NancyTheDreamtz Muda mchache baada ya kocha Jose Mourinho kutimulia ndani ya Manchester United, mchezaji ghali zaidi ndani ya timu hiyo Paul Pogba ameonesha kufurahishwa na uamzi huo. Kupitia mtandao wa Twitter Pogba ameweka picha iliyoambtana na ujumbe unaotaka wafuasi wake kuweka maoni yao juu ya picha hiyo. Hata hivyo Pogba aliifuta picha hiyo baada ya muda mfupi. Naye mkongwe wa klabu hiyo ambaye pia ni kocha, Gary Neville ameunga mkono ujumbe wa Pogba kwa kuuandika na kuweka kwenye ukurasa wake. Vyanzo mbalimbali pia vinataja makocha kadhaa ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Mourinho mwisho wa msimu huu baada ya klabu kuweka wazi kuwa kocha wa muda atakayetangazwa ndani ya saa 48 atadumu hadi mwisho wa msimu.

Kimenuka Diamond Afuta Picha zote za Mrembo Tanasha Instagram....Tanasha Afunguka Haya...

Image
NancyTheDreamtz Kimenuka Diamond Afuta Picha zote za Mrembo Tanasha Instagram....Tanasha Afunguka Haya huku na yeye pia akifuta picha zote alizowahi kipiga na Diamond... _ From #tanashadonna - Just to make things clear... D and I came to a mutual understanding that it may be too soon to be Kwanini Uteseke? Jipatie Dawa Bora ya Matatizo Mbali Mbali kwa Afya Yako with our relationship on social media right now. So we decided to keep our relationship private for the moment until we feel like going public again. May God bless you all .🙏❤️

Mbasha Amtolea Povu Zito Shabiki Alimwambia Anajichubua

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha amtole povu la kufa mtu shabiki yake katika mtandao wake wa instagram ambae anadai kuwa weupe wa Mbasha ni wa kujichubua. Mbasha amtolea uvivu shabiki huyo na kumpa za uso huku akimwambia kuwa weupe wake ni wa asili wala sio wa kuchakachua. Hiki ndicho alichoandika: hivi wewe unayenipakilia kwenye comment kwamba niache mkorogo nani alikwambia mie najicream sijawahi kujicream weupe wangu ni waasili waulize wanaonijua wakueleze, sawa na sura yako mbaya ilivyo ya asili domo kubwaa hata lipsi halina wanja sasa lipua kubwa kama bukta ya fudenge😀😀 macho kama mzeee wa likwidiii mamaanakufaa....kabala hujaniponda kwanza jiangalie wewe kwanza cheki mikorogo ilivyokukataaa jamani watu wa bongo muvi mkitaka kuigiza picha ya kutisha hapa kunajitu halihitaji hata mekapuuu.eti mamawatatu jamani haya mumfolo mkajionee @apoloniapeter12 kila siku unanipondaga tu navumilia haya leo Utajibeba

Diamond Platnumz Atishia Kuondoka Tanzania na Kuchukua Uraia Kenya

Image
NancyTheDreamtz Ameandika Ibrahim Augustine Mwimbaji maarufu na CEO wa WCB namzungumzia Diamond platnumz ametishia kuondoka Tz na kuhamia nchini Kenya hii ni kwa sababu nyimbo zake kufungiwa kila wakati na BASATA Maneno haya ameyasema kipindi akihojiwa na Times FM , nimekutana na Video Youtube Niki nukuu maneno yake "Mimi kama nyimbo zangu wataendele kuzifungia fungia hivi itabidi nisepe sasa wanataka tifa na mama yangu wale nini makaratasi?,mziki ndio ajira yangu naweza nikaenda hats Kenya na mambo yakawa fresh" Nini unajifunza Nimegundua kwamba msanii diamond anatumia cheo chake kikubwa ama wadhfa wake kuitishia BASATA Ili basata wamfungulie I swear wakifanya hivi wanaua vizazi kitu ambacho hakifai kwani hawezi kuimba nyimbo bila kuweka video au maneno ya matusi Mimi kama anataka asepe aondoke tena hata sasa hivi asituharabie maadili ya watoto wetu sasa hivi mitaani watoto wetu wanaongea maneno ya ajabu na machafu hata mbele za wageni (ila Mimi sijaoa na wale sina mke i...

Nape Nnauye: CCM Imevamiwa na Wasaka Tonge

Image
NancyTheDreamtz Na Bakari Chijumba, Mtwara. Wakati sakata la Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dr.Bashiru Ally na kada wa Chama hicho, Bernard Membe likiendelea kuchukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameibuka na kusema CCM imevamiwa na wasaka Tonge wenye maslahi na matumbo yao kuliko chama. Nape Nnauye ambaye ni mbuge wa Mtama, ametoa kauli hiyo baada ya kuenea kwa taarifa kuhusu madai ya  kuanzishwa kwa chama kipya kitakachoitwa USAWA, ambapo Bernard Membe na Nape Nnauye wametajwa kuwa miongoni mwa watakaotimkia kwenye chama hicho kipya. Taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa facebook unaofahamika kwa jina la "Sauti ya Kisonge" na kuenezwa kwenye mitandao hii leo, inadai Chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni, kinawahusisha pia  mawaziri kadhaa wa utawala uliopita, mawaziri wanne kutoka Zanzibar  na mabalozi kadhaa wastaafu na waliopo nje. "Chama Kipya kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni kwa jina...

IKULU Yampongeza Msanii Diamond...Mwenyewe Afunguka Maneno Mazito

Image
NancyTheDreamtz Baada ya ukurasa wa kijamii wa instagram wa Ikulu kumpongeza msanii Diamond Platnumz kwa mchango wake wa maendeleo ya jamii ikiwemo kuchangia shule ya msingi ya Sumbawanga katika ujenzi wake hatimaye mwanamuziki huyo ameandika ujumbe wa shukrani kwa Serikali  kwa kutambua mchango wake na sanaa kwa ujumla. Diamond ambaye kwa sasa yupo Sumbawanga kwaajili ya tamasha lake la Wasafi Festival, amekubali kubeba jukumu la kujitolea kuimalizia shule ya Msingi ya Sumbawanga ambayo ilihitaji milioni 68 ili kuhakikisha imemalizika na kuanza kupokea wanafunzi mwezi Januari ambapo aliridhia kubeba jukumu hilo huku akiongezea kuwa yupo tayari kujitolea na mabati 150. Advertisement

Angalia SABABU Ya Diamond Platnumz KUANGUKA JUKWAANI Huko SUMBAWANGA.

Image
NancyTheDreamtz

Diamond akiongea baada ya kuanguka jukwaani Sumbawanga

Image
NancyTheDreamtz