Posts

Tazama Hapa Video ya Navy Kenzo ft. Diamond Platnumz - Katika

Image
NancyTheDreamtz Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo wameachia video ya wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la  Katika  ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz. Itazame hapa. By Nancy Arthur Nyandiche

Papa Francis awatambua na kuwaridhia maaskofu saba walioteuliwa China

Image
NancyTheDreamtz Makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican na China zimetangaza juu ya kutiwa saini mkataba wa kihistoria, wa muda mfupi uliofikiwa kati ya pande hizo mbili kuhusu uteuzi wa maaskofu nchini China. Papa Francis amekubali uhalali wa maaskofu saba wa China, walioteuliwa na China bila idhini ya Vatican. Hatua hiyo imemaliza mzozo wa kidiplomasia uliokuwepo kwa miongo kadhaa na ambao umesababisha mgawanyiko miongoni mwa waumini wa Kikatoliki nchini China. Ni miongo saba sasa tokea Vatican na China zikate mahuasiano rasmi kati yao. Uamuzi huo ni sehemu ya makubaliano ya kihistoria kati ya Kanisa Katoliki na China juu ya uteuzi wa maaskofu, jukumu ambalo kwa kawaida huwa la Papa. Mkataba huo wa muda ulisainiwa mjini Beijing na kutangazwa wakati Papa Francis alipokuwa anafanya ziara nchini Lithuania ikiwa ni mwanzoni mwa safari yake ya siku nne katika mataifa yanayoizunguka bahari ya Baltic, kaskazini mwa Bara la Ulaya. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican, Papa Franc...

Sitaki kuolewa tena na kijana, nataka mwanaume mzungu aliyeachika – Hamisa Mobetto

Image
NancyTheDreamtz Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka wazi mwanaume ambaye anataka kuishi naye kwa sasa, ambapo amedai kuwa anataka mwanaume wa kizungu ambaye alishawahi kuachika na mwenye watoto. Hamisa Mobetto Akizungumzia vigezo vya mwanaume anayemtaka, Hamisa amesema kuwa kwa sasa hapendi kuolewa na vijana na anatafuta Mzungu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 45. “ Mimi hapa nataka labda mzungu au mtu mzima,  awe alishawaki kuachwa au Mgane kwa hiyo ndio hivyo, yaani nikisema kijana dah hapana. Awe angalau miaka 45 kwa sababu mimi mwenyewe nina watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wangu, “amesema Hamisa Mobetto kupitia EATV. Hamisa Mobetto tayari ameshazaa watoto wawili na wanaume wawili tofauti tofauti, ambao ni Diamond Platnumz na Majizzo na amesema kwa sasa hawezi kurudiana na yeyote kati yao. Kwa upande mwingine, Hamisa Mobetto amekiri kuwa sauti iliyosambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita akiongea na Mganga wa kienyeji...

Wamiliki wa Blog ya Dauda.com waachiwa kwa dhamana Mahakama ya Kisutu

Image
NancyTheDreamtz Wamilikiwa wa blog ya Dauda.com  wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mkazi Kisutu ambao ni pamoja na mtangazaji wa Clouds fm Shaffih Dauda. Wawili hao wanatuhimiwa kwa kosa la kuendesha blogs bila kuwa na kibali. Licha ya Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 mwezi wa kumi,washtakiwa hao walikataa tuhuma hizo za kumiliki blog bila kuwa na kibali. Wakili wa upande wa Jamhuri ameiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kwa Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambone ameiomba Mahakama kuwapa dhamana wateja wake kwa kuwa haki ya kupata dhamana ipo na Hakimu wa kesi hiyo amekubali kuwapa dhamana washtakiwa hao. Shafiih na wenzake ambaye anashikiliwa ni Ben Ali (Ben On Air) ambaye alikuwa muendeshaji wa Dauda TV kupitia mtandao wa (Youtube) walikamatwa wiki iliyopita kwa kosa la kuendesha blog hiyo bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Afya ya Haji Manara yatetereka, mwenyewe adai amelishwa sumu na sio presha ya matokeo ya Simba

Image
NancyTheDreamtz Baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameshikwa na presha iliyopelekea kulazwa mkoani Shinyanga, hatimaye mwenyewe aweka wazi kinachomsumbua. Haji Manara Manara amesema kuwa alikula chakula chenye sumu, na ndio sababu iliyompelekea kulazwa na sio presha ya matokeo mabaya ya klabu yake kama inavyoandikwa mitandaoni. “ Siumwi pressure wala moyo kama inavyoandikwa mitandaoni..nahic nimepata food poisoning na niwashukuru Madaktari walionihudumia awali Shinyanga na Mwanza ..now nisharejea Dar teyari kwa vipimo zaidi…Insha’Allah kila kitu kitazidi kuwa salama, “ameeleza Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram. Klabu ya Simba imekuwa na matokeo mabovu kwa msimu huu ambapo wiki iliyopita imepokea kichapo cha goli 1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Wanaharakati hawa watatu watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel wakiwa Jela

Image
NancyTheDreamtz Wanaharakati watatu wa haki za binadamu kutoka Saudia walioko jela watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel na taasisi ya Nobel mjini Stolkholm.Pia wapinga rushwa kutoka Guatemala watunukiwa tuzo ya heshima. Washindi wa tuzo maalum ya haki za binadamu au tuzo mbadala ya Nobel wametangazwa leo hii mjini Stolkholm Sweden. Tuzo hiyo imetunukiwa watetezi watatu wa haki za binadamu wakisaudi waliofungwa jela pamoja na wanaharakati wa kupinga rushwa kutoka Amerika Kusini. Taasisi ya tuzo hiyo mjini Stolkholm imesema dolla 113,400 zinazoambatana na tuzo hiyo mbadala ya Nobel zitagawanywa kwa washindi Abdullah al Hamid,Mohammad al-Qahtani na Waleed Abu al Khair wote wa Saudi Arabia kutokana na juhudi zao za kijasiri zinazosimamia misingi ya haki za binadamu ya kimataifa,ili kuleta mageuzi katika mfumo wa kidhalimu wa kisiasa nchini Saudi Arabia. Tuzo  ya heshima ya mwaka huu imetunukiwa Thelma Aldana wa Guatemala na mkolombia Ivan Velasquez kutokana na mchango wa...

Maua Sama na Soudy Brown kuendelea kusota mahabusu (Audio)

Image
NancyTheDreamtz Mwanamuziki Maua Sama Jumatatu hii hajapandishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa na wadau wengi huku wenzake Soudy Brown akipandishwa mahakamini na kusomewa shtaka moja la kutumia mitandao ya kijamii bila kuwa na kibali. Wawili hao kwa pamoja walikamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita kwa tuhuma za kuidhalilisha nembo ya Taifa baada ya kupost video moja mtandaoni inayowaonyesha watu wakichezea hela za Tanzania. SoudyBrown amesomewa shtaka moja la kuweka maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali lakini dhamana ya kosa hilo iko wazi lakini anadaiwa bado anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu. Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo Augustine Rwizile ameghailisha kesi hiyo hadi 18 October 2018. Naye Maua Sama hakuletwa mahakamani leo kama watu walivyotarajia huku wadau wa mambo wakidai kesi yake nitaanza kusikilizwa katikati ya wiki hii. Mmmoja kati ya mawakili ambao walijitokeza mahakamani hapo walidai wamewasiliana na jeshi la p...