Posts

Haya Hapa Matokeo ya Mpira Kati ya Tanzania na Uganda Jioni ya Leo

Image
NancyTheDreamtz Tanzania wanafanikiwa kurudi nyumbani na pointi 1 kwa sare tasa dhidi ya Uganda Cranes katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza mashindano ya African Cup of Nations 2019.

Flavian Matata Akutana na Nick Minaj Baada ya Kumpamba Kucha

Image
NancyTheDreamtz Baada ya Kupata Deal ya Kupamba Kucha za One of the Best female Rapper Kutokea Pande za Marekani @nickiminaj , Mwanamitindo Maarufu @flavianamatata amekutana nae na Kupata Picha ya Pamoja kwenye Tukio la Utolewaji wa Tuzo za #FMAS2018 August 21 Mwaka Huu, Flaviana Kupitia Account yake ya Twitter aliandika kuwa #NickiMinaj alitumia Product za Lavy Namba 29, wakati wa kupiga picha zilizotumika kwenye Jarida la Fashion la @voguearabia la Mwezi September Mwaka Huu

Rais Magufuli Asema Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka Ndo Anayeongoza Kwa Kuchapa Kazi Vizuri Tanzania Nzima..Makonda Je?

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtaja mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, kuwa ndiye mkuu wa mkoa kinara anayepiga kazi na kwamba hana mfano licha ya kupuuzwa kabla  hajamteua. Hayo ameyasema leo mkoani Simiyu wakati akihutubia wananchi wa mkoa huo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 katika mikoa ya kanda ya ziwa. Rais Magufuli ameeleza kuwa, wakati anajaribu kutafuta wakuu wa Wilaya na wakuu wa mikoa aliambiwa na vyombo vyake kuwa Mtaka hafai hata U-DC lakini yeye akaamua kumteua kuwa mkuu wa mkoa kwasababu anajua watu wazuri huwa wanapingwa vita sana. ''Nilipotaka kumteua niliuliza vyombo vyangu nikaambiwa hafai kabisa lakini nimeuliza ripoti ya Wakuu wa Mikoa wanaofanya kazi vizuri, wakaniletea Mtaka ndio namba moja na namba mbili ni yeye kwa kifupi hana mfano'', amesema. Aidha Rais Magufuli ambaye atakamilisha ziara yake katika mikoa hiyo siku ya Jum...

Masanja Mkandamizaji Aingia Katika Bifu Zito na Kanye West

Image
NancyTheDreamtz Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji amuwakia Rapper Kanye West hii ni baada ya kuandika ‘Sisi ni Miungu’ kupitia ukurasa wake wa twitter na wengi kutafsiri kuwa anajiita Mungu kitu ambacho sio kizuri. Masanja Mkandamizaji ambaye pia ni mchungaji amechukulia kitu hicho kuwa ni dharau na kusema mtu akishapata hela anasahau kama kuna Mungu na badala yake anajiita yeye Mungu. Kupitia ukurasa wa twitter wa Masanja ameandika mawazo yake kuhusiana na kile alichokiandika Kanye West na kusema “Acha Kuvuta bangi, huwa una umama sana”

Hiki ndicho alichokishutumu Obama kutoka kwa Trump akiuita ni “Upuuzi unaotoka White House”

Image
NancyTheDreamtz Aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama amemshutumu mrithi wake Donald Trump na mambo ya ‘kipuuzi yanayotoka’ katika ikulu ya Whitehouse. kwa kusema ”Hii sio kawaida huu ni wakati usio wa kawaida na ni wakati hatari”, Obama aliwaambia wanafunzi katika chuo kikuu cha Illinois. Alitaka kurejeshwa kwa uaminifu na heshima na sheria kufuatwa katika serikali, Rais huyo wa zamani amekuwa akifanya mambo yake kwa siri tangu alipoondoka mamlakani 2017. Bwana Obama aliambia sherehe hiyo ya kuwatuza wanafunzi mjini Urbana jimbo la Illinois kwamba amekuwa akitaka kufuata utamaduni wa marais wa zamani kupitia kuondoka katika ulingo wa kisiasa. Badala yake aliushutumu utawala uliopo wa Republican. Akimjibu, rais Trump alisema katika mkutano wa mchango wa Republican huko fargo kaskazini mwa Dakota siku ya Ijumaa kwamba aliitazama hotuba ya mtangulizi wake ,”lakini nililala”. ”Bwana Obama alijaribu kujipatia sifa ya mambo mazuri yanayoendelea nchini”, Wanachama wa Democr...

Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth afunguka kilichombeba ‘sijabebwa’

Image
NancyTheDreamtz Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth amefunguka mwanzo mwisho kile kilichopelekea kushinda taji hili la U-Miss kwa walikuwa wanashindana na warembo wengi halafu wazuri. Queen alisema “Nafurahia kushinda taji ili najisikia vizuri sana asante Tanzania” akiongeza “ukiwa kama mrembo lazima ujiandae kama unavyoona warembo ni wazuri sio kwamba ni wazuri kumuonekano tu hata kichwani pia wako vizuri” Hapa ndio maelezo yake:-

Hili ndio Swali la Mobetto lililompa ushindi Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth

Image
NancyTheDreamtz Mashindano ya Miss Tanzania yamemalizika kwa mrembo, Queen Elizabeth kutoka Zone ya Dar es salaam kuondoka na taji hilo huku akiwamwaga wenzake 19. Baada ya kuingia tano bora. Warembo hao waliulizwa na maswali na aliyejibu vizuri alijichukulia maski nyingi kutoka kwa majaji,kati ya warembo hao kuna wengine walijibu vizuri huku mmoja wao akipata kigugumizi wakati wa kujibu swali husika. N kati ya warembo hao warembo watatu walijibu maswali kwa lugha ya Kiingereza huku warembo wawili yaani aliyeshika nafasi ya tano na ya nne hao waliweza kujibu maswali kwa kutumia lugh ya taifa ya kiswahili huk mshindi namba tatu mpaka namba moja wakijibu kwa lugha ya kiingereza. Na haya ndio miongoni mwa maswali waliyoulizwa na hapa ndio mshindi wetu anajibu swali baada ya kuulizwa na mshereheshaji wa sherehe hiyo mwanamitindo Hamissa Mobetto.