Marekani: Baraza La Wawakilishi Lapitisha Mswada Wa Kuongeza Muda Wa Serikali Kukopa Fedha

Kevin McCarthy Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumatano liliidhinisha sheria ya kusimamisha ukomo wa kukopa kwa serikali, hadi mapema mwaka 2025, hatua inayoepusha mzozo wa kisiasa wa Washington, siku tano kabla ya nchi hiyo kufikia wakati ambapo ingekosa pesa za kulipa madeni yake. Katika kura hiyo ya Jumatano, wabunge 314 walipitisha mswada huo dhidi ya 117, walioupinga. Baada ya hapo, mswada huo sasa unaelekea kwenye baraza la Seneti ambapo utapigiwa kura kufikia mwishoni mwa wiki. Endapo utapitishwa na seneti, baraza ambalo linadhibitiwa na Wademokrat kwa wingi wa wajumbe, basi Rais Biden atautia saini na kuwa sheria. Hatua hiyo inasimamisha kiwango cha sasa cha deni la serikali la $31.4 trilioni. Wabunge wa chama cha RepubliKan wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, wamekosoa makubaliano yaliyofikiwa na Rais Mdemokrat Joe Biden na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mrepublikan Kevin McCarthy kwa kutopunguza vya kutosha, matumizi ya serikali ya siku za usoni, huku baadhi ya Wanademokrat wakitofautiana kuhusu suala hilo. nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais