Kocha Wa Manchester City Pep Guardiola Atwaa Tuzo Ya Kocha Bora Wa Mwaka Wa LMA

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Chama cha makocha wa Ligi. Hii ni mara ya tatu kwa Guardiola kutwaa Tuzo hiyo inayoitwa ‘Sir Alex Ferguson Award’, iinayopigiwa kura na mameneja ama makocha wa madaraja yote ya ligi nchini England. Mhispania huyo, 52, pia alishinda tuzo ya kocha ama meneja bora wa mwaka wa ligi kuu England baada ya timu yake kunyakua taji la tatu mfululizo na la tano katika misimu sita. Kocha wa Chelsea, Emma Hayes alishinda kwa upande wa Ligi ya Wanawake ya Super League. Ilikuwa tuzo yake ya nne mfululizo na ya sita kwa jumla. Guardiola amekuwa meneja wa tatu kushinda tuzo tatu au zaidi za kocha bora wa mwaka wa LMA, sawa na David Moyes, lakini bado yuko ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson mwenye tuzo 5. City watamenyana na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA Jumamosi. Ushindi katika mechi hiyo unaweza kuipa nafasi ya City kushinda makombe matatu msimu huu watakapomalizana na Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mnamo Juni 10, 2023. nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele