Kitumbo cha Tanasha Gumzo

NancyTheDreamtz
Kitumbo cha Tanasha Gumzo
GUMZO kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni muonekano mpya wa mpenzi wa mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch baada ya kuingia studio kisha kupiga picha zikimuonesha na kitumbo chake.

  Tanasha anatarajiwa kujifungua wakati wowote kuanzia sasa ambapo inaelezwa kuwa, sasa hivi ujauzito wake una miezi ipatayo nane na imembadili muonekano wake huku akipenda sana kulianika tumbo hilo.

Akizungumza na Amani, rafiki wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, mara ya mwisho kumuona laivu Tanasha alimshuhudia akiwa na tumbo kubwa na mara kwa mara alikuwa akijipiga picha za ukumbusho.


“Mimi nimemuona, kwa kweli mimba imemkubali na vile anavyojipenda sasa ndiyo amezidi kuwa ‘mtamu’, lakini anaonekana kuwa na kaugonjwa ka’ kujipiga picha. Kila wakati atapozi na kukuomba umpige picha huku akiweka mapozi tofauti,” alisema mtoa habari huyo.

Katika kudhihirisha kuwa Tanasha amekuwa na kaugonjwa ka’ picha, mwanadada huyo juzikati aliachia picha kadhaa akiwa amefunua tumbo lake, jambo lililoibua mjadala mtandaoni huku wengi wakisema anapita kulekule walikopita wapenzi wa zamani wa Diamond, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari’.

“Haah! Jamani umependeza sana my wii (wifi yangu), Mungu akujaalie ujifungue salama,” aliandika mmoja wa wachangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy Baby.

Mwingine akaandika: “Huyu anapita kulekule kwa akina Zari na Mobeto, kwani hawa mastaa hawaoni raha kujifungua bila kutuonesha matumbo yao? Ni ili iweje sasa.”


Aidha, mashabiki hao walienda mbele zaidi kwa kuwapambanisha Zari, Tanasha na Mobeto huku ikitakiwa ajulikane nani mimba ilimpendezesha na nani ana tumbo zuri la mimba.

“Nimeona matumbo ya Zari na Mobeto kipindi kile walipokuwa wajawazito lakini hili la Tanasha limenivutia, mimba haijamzeesha kabisa, zaidi amekuwa mzuri,” alikomenti Zulfa Mabiriani.


Mbali na mjadala huo mtandaoni, Tanasha hakujibu lolote zaidi ya kuzungumzia kuhusu baby shower (sherehe ya mama kabla ya kujifungua) yake kwa kusema anaisubiri kwa hamu kubwa.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele