Ufaransa Yapinga Matokeo ya Urais DRC

NancyTheDreamtz
Ufaransa Yapinga Matokeo ya Urais DRC
Ufaransa imepinga matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikisema ushindi uliotangazwa kwa kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi haulingani na matokeo ambayo mpinzani wake mkubwa, Martin Fayulu anaonekana kuupata.

Katika tamko lililotolewa jana baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian alisema Fayulu, ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili, ndiye aliyetakiwa kutangazwa mshindi.

"Kwa kweli inaonekana matokeo yaliyotangazwa, hayaendani na matokeo halisi," alisema alipozungumza na kituo cha televisheni cha CNews.

"Kwa kuangalia (matokeo halisi), Fayulu ndiye kiongozi aliyepatikana katika uchaguzi huu. "

Alisema Kanisa Katoliki, ambalo lina wafuasi wengi na ambalo lilituma waangalizi 40,000, linajua nani hasa aliyehinda na maoni yao yanaonyesha mshindi ni Fayulu.

"CENCO ilifanya ukaguzi na kutangaza matokeo ambayo yalikuwa tofauti," alisema akimaanisha baraza la maaskofu la Kanisa Katoliki.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele