China Waridhia Mkutano wa Pili Kati ya Kim Jong-un na Trump mara ya pili

NancyTheDreamtz
China Waridhia Mkutano wa Pili Kati ya Kim Jong-un  na Trump mara ya pili
Baada ya kutembelea gafla China, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameondoka akiwa anaungwa mkono juu ya uwezekano wa kukutana tena na Rais wa Marekani Donald Trump, televisheni ya taifa iliripoti.

Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza mwezi June, lakini maendeleo kuhusiana kuondokana na namatumizi ya nyuklia yalileta matumaini.

Rais wa China Xi Jin Ping amesema ana matumaini viongozi hao wawili watakutana nchi yoyote yoyote ambayo si Marekani wala Korea Kaskazini, shirika la habari la Xinhua linaripoti.

China ndio rafiki na mshirika mkubwa Korea Kaskazini. Nchi mbili hizo zina mahusiano makubwa na imara ya kibiashara.

Xi amesema nchi yake inaunga mkono mkutano wa Korea Kaskazini na Marekani na anaunga mkono pande hizo mbili kujadili tofauti zao kwa mazungumzo.

Pia amesema China itakuwa tayari kushika jukumu chanya la kulinda amani na hatimaye kufikia lengo la kuondoa nyuklia katika rasi ya Korea, Xinhua inaripoti.

Treni inayoaminika kumbeba kiongozi wa Korea Kaskazini, ikiondoka katika kituo cha treni Beijing.
Katika ugeni huo wa siku tatu nchini China, Kim na mke wake Ri Sol-ju walikaribishwa na Rais wa China Xi na mkewe kwa maua na burudani. Pia alitembelea kiwanda cha dawa kinachotengeneza dawa za za asili za Kichina.

Xi alikubali mwaliko wa kuitembelea Korea Kaskazini, kwa mujibu wa vyombo vya habari. Lakini haijajulikana lini atafanya hivyo.

'Hofu' juu ya kuondoa silaha za nyuklia

Katika hotuba yake ya mwaka mpya, Kim alisema bado ana mpango wa kuondoa silaha za nyuklia, lakini akaonya kuwa atabadili mawazo yake kama vikwazo vya Marekani vitaendelea.

Kwa mujibu wa shirika la Korea Kaskazini KCNA China inaunga mkono msimamo wa nchi hiyo.

Haijawekwa wazi ni lini na wapi mkutano tarajiwa wa Kim na Trump utafanyika, japokuwa rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alisema utatokea hivi karibuni.

Bwana Moon ambaye kwa mwaka mzima alikuwa akifanya kazi ya usuluhisho kati ya Korea Kaskazini na Marekani, alisema katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi kuwa Seoul itashirikiana na Marekani kutatua suala la vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Korea Kaskazini

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele