Tajiri Namba Moja Duniani, Jeff Bezos Wamwagana na Mkewe wa ndoa, Skendo za Usaliti Zahusishwa

NancyTheDreamtz
Tajiri Namba Moja Duniani, Jeff Bezos Wamwagana na Mkewe wa ndoa, Skendo za Usaliti Zahusishwa

Jeff Bezos na mkewe


Tajiri namba moja duniani, Jeff Bezos wamwagana na mkewe wa ndoa, skendo za usaliti zahusishwa
Godfrey Mgallah  19 hours ago 1,062
FacebookTwitterShare via Email



Afisa Mtendaji Mkuu na mwanzilishi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos na mkewe MacKenzie wamepeana talaka baada ya kuishi miaka 25 kwenye ndoa.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wawili hao kwenye mtandao wa Twitter, wameeleza kuwa watabaki kuwa marafiki biashara na kulea watoto pamoja.

“Baada ya kuishi kipindi kirefu cha misukosuko na kujaribu kutengana, hatimaye tumeamua kuachana na kuendelea na maisha yetu kama marafiki,“imeeleza taarifa hiyo.

Ni miaka miwili sasa imepita tangu wawili hao waingie kwenye mifarakano, baada ya skendo ya Jeff kumsaliti mkewe kwa mwanamke wa rafiki yake Patrick Whitesell aitwaye Lauren Sanchez.

Wakati hayo yakijiri bado kampuni ya Amazon iliyoanzishwa miaka 25 iliyopita, imeendelea kufanya vizuri kimauzo. Kwani ripoti iliyotolewa na Forbes imeeleza kuwa Amazon ndio kampuni yenye thamani kubwa zaidi 2019 duniani, ikiizidi Microsoft .

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele