Fahamu jiwe la ekari 7 lenye ramani ya bara la Afrika linalotumika katika ibada za kimila Tanzania

NancyTheDreamtz

Huwenda umepata kusikia maajabu mengi duniani hebu fahamu na hili, huko Mkoani Njombe Kusini Magharibi mwa nchi ya Tanzania kuna jiwe kubwa kwa jina la Lwiwala lenye ramani ya bara la Afrika.

Jiwe hilo la ukubwa ekari 7.8 limejizoelea umaarufu mkubwa kutokana na kuwepo kwa ramani ya bara la Afrika ambayo haijachorwa na mtu.

Katika mahojiano yake na Shirika la habari la BBC Mhifadhi Msitu wa Lwiwala, Yuda Masamaki amesema kuwa wakazi wa kijiji hicho hulitumia jiwe hilo katika ibada za kimila.

”Limepewa jina Lwiwala kwa sababu humeremeta nyakati za usiku, baadhi ya wakazi hutumia jiwe hilo kama madhabahu ya ibada zao za kimila,” amesema Yuda Masamaki ambaye ni Mhifadhi Msitu wa Lwiwala.

Masamaki ameongeza ”Humu kuna ramani ya Afrika ambayo haijachongwa na wanakijiji, isipokuwa ilitambuliwa na wataalamu.”


Jiwe hilo lenye ramani ya Afrika maarufu kama Lwiwala hutembelewa na watalii mbalimbali huku wageni wakitozwa dola 25 za Kimarekani huku wazawa dola mbili pekee.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais