RC Makonda Amtaka Majizzo Afunge Ndoa na Lulu Haraka

NancyTheDreamtz
RC Makonda Amtaka Majizzo Afunge Ndoa na Lulu Haraka
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amefunguka na kumtaka mkurugenzi wa EFM, Majizzo afunge ndoa na msanii Elizabeth Michael haraka iwezekanavyo la sivyo atamfunga.

RC Makonda amefunguka hayo Kwenye mazungumzo na waandishi wa habari kwenye tamasha la Komaa Concert jana jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kutokana na imani yake hataki kuwaona marafiki zake wanakuwa mabachela na kuahidi kuwafunga jela endapo watakiuka ahadi zao za kuoa.

Marafiki zake aliwataja na kuwataka waoe mara moja ni pamoja na Majizzo, Leo Mutuz, Meya wa Kinondoni na kuhaidi kuwafunga endapo hawatafanya hivyo.

Nina ndoa kubwa tatu lazima nizisimamie na wasipooana nawafunga, moja ni Majizzo unajua mimi ni mkristo kwenye Biblia inasema wengine wataokolewa kwa moto. Sasa Majizzo tayari yupo kwenye mipango na binti yangu Lulu wameshakuja nyumbani tumeshafanya vikao vingi vya kupanga harusi.

Lakini kuna harusi nyingine ya Meya wa Kinondoni nimemwambia na yeye asipooa namfunga. Lakini kuna Lemutuz naye asipooa namfunga. Kwa hiyo kuna watu watatu hawa lazima mipango yao ya harusi ikamilike mwaka huu na waoe”.

Tangu Lulu atoke jela Kumekuwa na tetesi kuwa yeye na mpenzi wake Majizzo wapo katika mipango ya kufunga ndoa na hata Makonda alikuwa wa kwanza kutangaza Ndoa hiyo. 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele