Sikuwahi kuolewa, najua tunakokwenda wanawake watakuwa na nguvu kuliko akina baba – Mh. Anne Makinda (+video)
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
-
NancyTheDreamtz
Aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Anne Makinda ameelezea historia yake fupi ya maisha toka enzi anasoma hadi kuja kufanikiwa kuwa kiongozi mkubwa bungeni.
Mhe. Anne Makinda
Mhe. Makinda amesema maisha yake yote yalikuwa bungeni na kipindi hicho amesema kuwa alikuwa na fujo sana kuliko hizi ambazo zinafanywa na baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani bungeni.
“Mimi maisha yangu yote yalikuwa bungeni, mimi mwenyewe kama kuwa mtu wa fujo i was of those.. nilikuwaga backbencher nilikuwa na fujo nawambia ndugu zangu akina Tundu Lissu kuwa kwanza nyie hamuwezi kunifikia mimi,“amesema Anna Makinda.
Akielezea upande wa mahusiano Bi. Makinda amesema yeye hakuwahi kubahatika kuolewa na amewaasa wanawake waliokwenye ndoa kuwa makini sana pale wanapopata mafanikio kwani ndio kipindi cha kushirikiana karibu sana na wanaume zao ili kufika mbali.
“Mimi sikuwahi kuolewa lakini nilipopata mtoto wangu, aliyenisaidia sana ni dada yangu. Kwa hiyo nikiwa shuleni tu IDM nikipata ile shilingi 20 kumi napeleka kwa dada, 10 nabaki nazo kwa hiyo toka huko nilikuwa nafanya kazi I have to survive .“amesema Bi. Makinda na kusisitiza jambo kwa wanawake walioolewa.
“Tunakokwenda najua kabisa akina mama watakuwa na nguvu zaidi kuliko akina baba, na ndio maana nawa-advice pia tujifunze kuwapenda hawa watu. Kwa sababu kama wewe ni Couple umeolewa halafu unakuwa successful kuliko mume wako, usipoweza kumeneji hiyo anaweza kukuharibia hata wewe, ni vizuri kumshirikisha ikawa ile successful yako ikawa ni part ya familia yako au successful ya couple yenu,“amesema Anne Makinda akielezea historia yake kwenye mahojiano na TGNP Mtandao, tazama video hapa chini.
Mhe. Anne Makinda ndiye mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alishawahi kuhudumu pia kwenye shirika la UNICEF .
NancyTheDreamtz Huu kwa mujibu wa utafiti wa kabila zilizotoa wasomi wengi nchini tanzania. 1.wahaya wanapatikana mkoani kagera wakitokea bukoba na sehemu zingine za mkoa huoo 2.wagitaa wanapatikana wilaya ukerewe na musoma mjini na vijini mkoani mara 3.wachaga mkoani kilimanjaro wa wilaya ya moshi mjini,marangu,hai na sehemu zingine 4.wanyakyusaa mkoani mbeya wapo haswa wilaya ya kyela,songwe na zinginezo. 5.wakurya mkoani mara wilaya ya tarime na serengeti 6.wajaluo mkoani mara wilaya ya rorya na serengeti pia 7.wangoni wanatokea mkoa wa ruvuma 8.wapare wanatokea mkoa kilimanjaro wilaya ya same. 9.wasukuma hawa wapo mwanza na shinyanga 10.wanyamwezi hawa wanatokea mkoani tabora
NancyTheDreamtz Jeshi la Uganda limezindua mifuko ya kondomu katika kambi yake ya kijeshi ya UPDF Bombo iliyopewa kibwagizo cha usiende nyama kwa nyama. Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Brigedia Leopoldo Kyanda amesema mwanajeshi hawezi kutekeleza wajibu wake ipasavyo bila wenyewe kujilinda kutokana na maambukizi ya zinaa na hususan virusi vya ukimwi. Kondomu hizo zimepewa jina Ulinzi na zinatarajiwa kusaidia katika juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vinavyosababisha Ukimwi. Kitengo cha kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi jeshini kilizindua nembo hiyo mpya kwa ushirikiano na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali.
Comments