Irene Uwoya Ageuka Mbogo Baada Ya Kuulizwa Kuhusu Dogo Janja

NancyTheDreamtz
Irene Uwoya Ageuka Mbogo Baada Ya Kuulizwa Kuhusu Dogo Janja
Msanii wa filamu za Bongo Movie Mrembo Irene Uwoya amemwaga povu zito baada ya kuulizwa sababu za kutomposti mume wake Staa wa Bongo fleva Dogo Janja Kwenye kitandani zake za mitandao ya kijamii.

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja hawana maelewano na tetesi hizo zimezidi baada ya wawili hao kutopostiana Kwenye social media kama siku za nyuma.


Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Uwoya amemwaga povu na kudai  kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi.

Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya”.

Lakini pia Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake.

Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone”. 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele