Hivi Ndivyo Wema Sepetu Alivyowafunika wasanii wa kike wa Tanzania

Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amekuwa msanii wa kwanza kwa wanawake Tanzania kufuatiliwa na watu wengi zaidi ya milioni 3.7 kupitia mtandao wa Instagram, huku nafasi ya pili ikishikwa na Jackline Wolper ambaye ana followers milioni 3.4.

Nafasi ya tatu imeshikwa na Vanessa Mdee ambaye ana followers milioni 3.3, akifuatiwa na Shilole mwenye 'followers' 3.2 huku Linah Sanga akishika nafasi ya tano kwa 'followers' milioni 2.8.

Hayo yamebainika baada ya utafiti uliofanywa na www.eatv.tv kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram leo Agosti 16, 2018, wenye lengo la kutaka kufahamu ukubwa wa majina waliyokuwa nayo wasanii hao kama unafanana na idadi ya watu wanaofuatilia na kuwakubali mitandaoni, licha ya watu hao kuwa wanatoka maeneo mbalimbali ya miji.

Mbali na hao, muigizaji Elizabeth Michael (LULU) ameshika nafasi ya sita kwa 'followers' milioni 2.6, mkongwe wa bongo fleva, Lady Jay Dee maarufu kama 'Komando Jide' ameshika nafasi ya saba akiwa na followers milioni 2.3, nafasi nane ikichukuliwa na muigizaji Shamsa Ford akiwa na 'followers' milioni 2.2 huku nafasi ya tisa ikichukuliwa na muigizaji Irene Uwoya akiwa na 'followers' milioni 1.7.

Nafasi ya 10 ikifungwa na Snura akiwa na milioni 1.5 ya watu ambao wanafuatilia kazi zao na vitu vingine mbalimbali kutoka katika kurasa zao za Instagram.

Wengine ni Nandy akiwa na laki 930, Mwasiti laki 798, Ruby akiwa na laki 491, Maua Sama laki 465, Chemical mwana wa Lubao akiwa na laki 354, Rosa Ree laki 327

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele