Binti Aliyetaka Kujiua Apata Nafasi Nyingine ya Kuishi Baada ya Kupandikizwa Sura

Binti aliyetaka kujiua apata nafasi nyingine ya kuishi baada ya kupandikizwa sura
Katie Stubblefield alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipopata majeraha makubwa baada ya kupigwa risasi.

Aliokolewa maisha yake hospitalini ingawa majeraha aliyoyapata yalimfanya msichana huyu maisha yake yabadilike na muonekano wa uso wake ulikuwa umebadilika karibu wote.

Kwa sasa msichana huyo ana umri wa miaka 22 na ameweza kuonyesha matokeo ya upandikizaji wa uso wake ulichukua miaka kadhaa katika jarida la 'National Geographic'

Chapisho hili lilipata nafasi ya kipekee katika kilniki ya Ohio ambayo ilimfanyia upasuaji binti huyo wakati akiwa ana umri wa miaka 21.

Waandishi wa habari na wapiga picha walifuatilia upasuaji huo tangu maandalizi yanaanza mpaka wakati wa upasuaji ambao ulitumia muda wa saa 31.

Picha ya sura ya Katie ambayo ipo juu ya jarida hilo la mwezi wa septemba iliweza pia kusimuliwa katika Makala ya kwenye mtandao.

Mpaka sasa ni watu 40 tu ndio wameweza kubadilishwa muonekano wa sura zao.Mtu wa kwanza kufanyiwa upandikizaji huo ilikuwa mwaka 2010 na alifanyiwa na daktari kutoka Uhispania.

Kwa kuwa upasuaji huu bado unafahamika kama ni majaribio hivyo basi malipo yake hayapo kwenye bima nchini Marekani.

Upasuaji alioufanya Katie ulidhaminiwa na taasisi ya 'Armed Forces'ambayo inataka kuboresha matibabu ya askari ambao watakuwa wamejeruhiwa katika vita.

Katie aliaminika kuwa ni mtu sahihi kufanyiwa jaribio hilo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo pamoja na umri wake.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele