Posts

Mserbia Yanga SC Ampa Shavu Carlinhos

Image
KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu. Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1. Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti. “Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani. “Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” alisema kocha huyo. Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo ...

Mastaa Hawa Wamefunikana Kwelikweli Kwenye Ligi

Image
TAYARI kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kimeanza ambapo timu nyingi kwa sasa zimeanza kusaka pointi tatu ndani ya uwanja kwa msimu wa 2020/21. Mabingwa watetezi ni Simba, walitwaa taji hilo msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kujiwekea kibindoni pointi 88. Tayari Septemba 6 walikiwasha huku na watani zao wa jadi Yanga nao walikiwasha pia.Simba wao walikuwa Uwanja wa Sokoine kumenyana na Ihefu ambapo ilishinda mabao 2-1, Yanga wao walijiwekea ngome pale Uwanja wa Mkapa na ilitoshana nguvu kwa safari yake imeanza ndani ya Uwanja wa Sokoine na ana kazi ya kukiongoza kikosi chake kutetea taji la Ligi Kuu Bara. Bocco aliyeyusha dakika zote 90 na alikiri kwamba Ihefu FC sio timu ya mchezomchezo ndani ya ligi licha ya kwamba ni msimu wake wa kwanza. JOASH ONYANGO Licha ya kwamba hakuwa na chaguo wakati akishuhudia shuti la Omary Mponda likizama ndani ya nyavu za kipa wake Aishi Manula, Onyango alipambana. Kazi kubwa ilikuwa ni kuokoa hatari za Jordan John ambaye alikuwa ni msumbuf...
Image
Msemaji wa Simba, Haji Manara jana alikuwa kivutio kwenye Tamasha la Simba Day baada ya kupanda jukwaani la kucheza Yope wimbo wa mwanamuziki Diamond Platniumz na Mkongomani Innos’B. Tamasha hilo lilifanyika Uwanja wa Mkapa, Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki ambapo Diamond na kundi lake la WCB walipiga bonge la shoo kabla ya mechi ya timu hiyo na Vital’O ya  Burundi. Katika tukio hilo kundi hilo likicheza wimbo huo Manara naye aliavamia jukwaa na kuanza kuwanogesha mashabiki kwa kucheza sambamba na wasanii hao. Kwa jinsi jamaa alivyokuwa akienda sambamba na wanasanii hao ilikuwa ni kama walifanya mazoezi ya pamoja na hivyo kuzua shangwe za kumshangilia. NancyTheDreamtz

CCM YA 2020 INAONYESHA UKOMAVU KWA KUFANYA UCHAGUZI WA UMOJA WA VIJANA

Image
    Chama Cha Mapinduzi kimezidi kuonyesha ukomavu kwa kufanya Uchaguzi ulio Thabiti nakuweza kupata wabunge wa viti maalumu UVCCM kupitia mchakato vijana walionyesha ukomavu kwa Vijana na kufanikiwa kuwapata wawakilishi hao bila kulipua hata kidogo                                              NancyTheDreamtz

UMAWEZA BADO INAENDELEA KUONYESHA UIMARA WAKUKZA ELIMU YA SAYANSI VISIWANI ZANZIBAR

Image
      Ilikuonyesha dhamira ya dhati katika kuipa morali jamii ya Zanzibar Taasisi ya Umaweza imeonyesha uimara zaidi katika maonyesho ya Nanenane visiwani humo kwa kuonyesha bidhaa zinazoweza kumfanya Mwanafunzi kuwa imara katika elimu ya sayansi kwakuweka vitendea kazi vinavyoweza kumpa Mwanafunzi uelewa zaidi wakisayansi kama uonavyo picha hapo chini                                            NancyTheDreamtz

UNASUMBULIWA na Fangasi za Sehemu za Siri...? Usijali Zingatia Haya Kujitibu Bila Gharama Yeyote Ile..!!!

Image
Ugonjwa wa fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea vijulikanavyo kwa kitaalamu kama ‘Candida albicans’. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote lakini hushambulia zaidi wanawake sababu ya maumbile yao ya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinachopelekea wao kuathiriwa zaidi kuliko wanaume. Watu karibu wote tunaishi na vimelea hivi katika miili yetu kwa kiwango kidogo sana. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria wazuri wa mwili ndiyo kupambana na vimelea hivi hata unaona huuguwi ila kinga ya mwili ikiyumba kidogo na bakateria wabaya kuongezeka ndipo hapo unapokutana na ugonjwa kamili. Tatizo la kuwashwa sehemu za siri ni tatizo kwa watu wengi miaka ya sasa na linawapata watu wa jinsia na rika zote yaani watoto, vijana hata wazee. Fangasi siyo sababu pekee ya kuwashwa sehemu za siri, kuna sababu na magonjwa mengine yanahusika na tatizo hili na kupona au kuondoka kwa sababu hizo ndiyo kupona kwa huo muwasho. Sababu za muwasho sehemu za siri za mwanaume Sababu zifuatazo zinaweza kuh...

Ibraah Tz "Siwezi kuwa na Jacqueline Wolper"

Image
Msanii wa lebo ya Konde Gang Music Ibraah Tz "Chinga" amesema hawezi kuwa kwenye mahusiano na Jacqueline Wopler kwa sababu anamchukulia kama mama yake japokuwa Harmonize alimpigia pande ili awe nae kwenye mahusiano.  Akizungumzia suala hilo la kupigiwa pande na Harmonize ili awe kwenye mahusiano na Wolper, Ibraah Tz amesema anamchukulia msanii huyo wa filamu kama mama yake na yeye bado yupo single.  "Ule ulikuwa ni utani tu unajua kuna muda kaka natakiwa ni-enjoy naye, haiwezi kuwa mimi nitoke na Jacquline Wolper yule ni mama yangu ananisapoti kwa hiyo namshuru sana sapoti yake ni kubwa kwangu, bado sina mahusiano nikiwa nayo nitaweka wazi na watu watajua" ameeleza Harmonize " NancyTheDreamtz