Msemaji wa Simba, Haji Manara jana alikuwa kivutio kwenye Tamasha la Simba Day baada ya kupanda jukwaani la kucheza Yope wimbo wa mwanamuziki Diamond Platniumz na Mkongomani Innos’B.

Tamasha hilo lilifanyika Uwanja wa Mkapa, Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki ambapo Diamond na kundi lake la WCB walipiga bonge la shoo kabla ya mechi ya timu hiyo na Vital’O ya  Burundi.



Katika tukio hilo kundi hilo likicheza wimbo huo Manara naye aliavamia jukwaa na kuanza kuwanogesha mashabiki kwa kucheza sambamba na wasanii hao.



Kwa jinsi jamaa alivyokuwa akienda sambamba na wanasanii hao ilikuwa ni kama walifanya mazoezi ya pamoja na hivyo kuzua shangwe za kumshangilia.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele