Posts

Mwijaku Aampa Ushauri Hamisa Mobetto " Ulifanikiwa Kuchomoka, Ukapona! Kuwa Makini, Usiangukie Kwenye Mikono yao Tena"

Image
NancyTheDreamtz Ujumbe wa Mwijaku kwa Hamisa Mobeto "Wataanza Kukumiss pale watakapokosa mbadala wako. Wataanza kukumiss pale watakapoona uso wako umejaa tabasamu na muonekano wako ni bomba kuliko awali. Ulifanikiwa kuchomoka, ukapona! Kuwa makini, usiangukie kwenye mikono yao tena"

Koffi Olomide Amwagia Sifa Kibao Mwanamuziki Nandy

Image
NancyTheDreamtz Kupitia kwenye kipindi cha Jahazi kinachorushwa Radio Clouds FM nguli wa muziki wa dansi 💥Koffiolomide amefunguka na kusema anakubali uimbaji wa NANDY KOFFI ALISIKIA NA KUSEMA Kuna msanii wa kike huyo nani kaimba kivuruge, oooh nandy namkubali'- Koffi Olamide Kabla sijarudi congo inshallah tutafanya jambo Tanzania ni nyumbani'- Koffiolomide

Jokate Awataka Yanga Kujaza Taifa Waiue Simba

Image
NancyTheDreamtz Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegello. MMOJA wa wapenzi maarufu wa Yanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegello, amewataka wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati watakapopambana na watani wao wa jadi, Simba. Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao Yanga ndio watakaokuwa wenyeji, unatarajiwa kupigwa kesho saa 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Ikumbukwe katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo uliisha kwa sare ya mabao 2-2. Simba waliongoza kwa mabao 2-0 kabla ya Yanga kupambana na kuchomoa yote ndani ya dakika saba. Akizungumza na Championi Jumamosi, Jokate alisema Yanga watashinda mchezo huo wa Jumapili kutokana na ubora wa kikosi chao. “Sina wasiwasi na timu yangu ya Yanga, naamini itashinda tu mbele ya Simba, niwaombe mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi uwanjani wakiwa wamevaa jezi za timu yetu ili wawape morali wachezaji wetu waweze...

Katibu Mkuu CCM: Tutatumia Dola Kubaki Madarakani

Image
NancyTheDreamtz Katibu  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, amekiri chama chake kuitumia dola kuhakikisha kinabaki madarakani. Amesema kama chama chochote kinachoongoza serikali kitashindwa kutumia dola kubaki madarakani, utakuwa uzembe wa chama chenyewe. Kwa kulitambua hilo, Dk. Bashiru amesema CCM imekuwa ikitumia dola kujihakikishia ushindi wakati wa uchaguzi na mwaka huu wamepanga "kuitumia dola kweli kweli". Lakini, kiongozi huyo wa CCM akaonya kuwa chama kinachoongoza serikali, hakipaswi kuitumia dola kunyanyasa wapinzani wake. Dk. Bashiru aliyasema hayo katika mahojiano maalum na vyombo vya habari vya IPP alivyovitembelea jijini Dar es Salaam jana. "Ukishakuwa chama tawala, kuna dhana inaitwa nafuu ya mwenye madaraka. Ukishindwa kutumia nafuu hiyo, utakuwa kama KANU (chama tawala cha zamani cha Kenya), iliposhindwa kutumia nafuu hiyo, haikuwahi kurudi madarakani au UNIP ya Zambia. "Unashika dola halafu unatumi...

Senegal na Tunisia Zathibitisha kuwa na waathirika wa corona

Image
NancyTheDreamtz Senegal na Tunisia zimethibitisha kuwa na waathirika wa corona.  Waziri wa afya wa Senegal Bw. Abdoulaye Diouf Sarr amesema mgonjwa aliyeambukiziwa ni raia wa Ufaransa, baba wa watoto wawili, alirudi Dakar mnamo tarehe 26 mwezi Februari kutoka Paris kwa ndege ya Senegal, baada ya safari ya mapumziko kusini mwa Ufaransa. Tarehe 28 mwezi Februari, idara ya afya ya Ufaransa iliarifiwa na zahanati binafsi kuwa mtu mmoja alionyesha dalili za COVID-19, baadaye alithibitishwa kuambukizwa COVID-19 katika Taasisi ya Pasteur mjini Dakar, lakini hali yake sio mbaya, na familia yake imewekwa kwenye karantini. Waziri huyo amewataka raia wasichanganyikiwe, na kuchukua hatua za kujikinga zinazotangazwa na wizara ya afya.     Mgonjwa aliyebainika Tunisia ni Raia wa Tunisia ambaye ametokea Italy. Nchi zenye Watu wenye virusi hivyo kwa Afrika zimefikia tano, nyingine ni Algeria,Misri na Nigeria

Vijana 11 Wakamatwa Kwa Utapeli wa Ile PESA Tuma Kwenye Number Hii

Image
NancyTheDreamtz Jeshi la Polisi linawashikilia vijana 11 wenye umri wa kati ya miaka 20 - 25 kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi kupitia Mtandao wa Facebook kwa kutumia majina ya viongozi wa Serikali na Wasanii maarufu Wanadaiwa kuwa walikuwa wakishirikiana na Mawakala wa kusajili laini za simu kupata laini zilizosajiliwa kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzitumia kutapeli watu kwa kuwatumia jumbe fupi za simu zinazosema 'Ile pesa tuma kwenye namba hii' Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema vijana hao walifungua akaunti Facebook zenye majina ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo -

Meneja wa GRAMMY Ashangazwa na Uwezo Pamoja na Uthubutu wa Diamond Platnumz

Image
NancyTheDreamtz Moja ya mameneja wa muziki duniani na mfanyakazi anayefanya kazi kwenye ofisi za waandaji tuzo za Grammy @marlonfuentes ameshangazwa na uwezo wa Diamond Platnumz baadabya kuudhuria kwenye show ya Diamond iliyofanyika kwenye Los angels Marekani Kabla ya kuudhuria show hiyo meneja huyo alitembelewa ofisini kwake na Diamond Platnumz akiwa na uongozi wake na kuzungumza mambo mawili matatu kuhusu muziki. Meneja huyo ameahidi kuwa kuna uwezekano mkubwa kumuona Diamond kwenye tuzo za Grammy hivi karibuni HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG < DOWNLOAD HAPA > Meneja huyo ameonesha kufurahishwa na uwezo wa Diamond katika kuwapa mashabiki kile wanataka na amemwita 'Mmoja wa wasanii wakubwa duniani kutoka Tanzania'. MARLON alishawahi kuwa Dj wa mwanamuziki Shakira .