Posts

Ufaransa Yapinga Matokeo ya Urais DRC

Image
NancyTheDreamtz Ufaransa imepinga matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikisema ushindi uliotangazwa kwa kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi haulingani na matokeo ambayo mpinzani wake mkubwa, Martin Fayulu anaonekana kuupata. Katika tamko lililotolewa jana baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian alisema Fayulu, ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili, ndiye aliyetakiwa kutangazwa mshindi. "Kwa kweli inaonekana matokeo yaliyotangazwa, hayaendani na matokeo halisi," alisema alipozungumza na kituo cha televisheni cha CNews. "Kwa kuangalia (matokeo halisi), Fayulu ndiye kiongozi aliyepatikana katika uchaguzi huu. " Alisema Kanisa Katoliki, ambalo lina wafuasi wengi na ambalo lilituma waangalizi 40,000, linajua nani hasa aliyehinda na maoni yao yanaonyesha mshindi ni Fayulu. "CENCO ilifanya ukaguzi na kutangaza matokeo ambayo yalikuwa tofauti," alisema akimaanisha baraz...

RC Makonda Awahimiza Wananchi Kujiunga Na Rais Magufuli Kuipokea Ndege Ya Sita Ya Serikali Airbus A220-300 LEO Mchana

Image
NancyTheDreamtz Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika Wananchi wote Wapenda maendeleo kujiunga na Mtekelezaji namba moja wa Ahadi Rais Dkt. John Magufuli kwenye mapokezi ya Ndege ya Sita ya Serikali (Airbus A220-300) itakayowasili Nchini leo January 11 Saa sita Mchana ikitokea Nchini Canada. Hafla ya mapokezi itafanyika kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Rais Magufuli aliahidi na sasa anatekeleza WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA Post By NancyTheDreamTz Girl

Kudanga since Ishu kwangu Ila Kama Kunamtu Anafanya Hivyo kwa Kufanya Jambo la Maana Haina Tatizo- Faiza

Image
NancyTheDreamtz MWIGIZAJI wa filamu Bongo na mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya-Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally ameeleza kuwa kudanga kwake siyo ishu kwani kama mtu anafanya hivyo kwa kufanya kitu cha maana siyo tatizo. Akipiga stori na Ijumaa, Faiza alisema kama ni kudanga amedanga, lakini alifanya hivyo kwa malengo fulani kwa sababu hakuna anayependa kudanga, alipotatua shida yake kwa sasa amekuwa shujaa na anayejitokeza na kumcheka hajitambui. “Nilidanga kwa sababu zangu nilizokuwa nazo na mwisho wa siku naendelea na maisha yangu,” alisema Faiza.

Mkoba Uliojaa Mamilioni Hela za Mugabe Yaibiwa

Image
NancyTheDreamtz WATU watatu wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe, wakishtakiwa kuiba mkoba uliokuwa na Dola za Marekani 150,000 (Sh. milioni 345) taslimu mali ya rais wa zamani wa taifa hilo, Robert Mugabe. Washukiwa hao wa wizi wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo. Jamaa wa rais huyo wa zamani, Constantia Mugabe, ni miongoni mwa walioshtakiwa, kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya serikali. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na funguo za nyumba ya kijijini ya Mugabe iliyo eneo la Zvimba karibu na mji mkuu wa Harare, na ndiye aliyewasaidia hao wengine kuingia humo na kufika ulikokuwa mkoba huo. Washukiwa hao wengine walikuwa wameajiriwa kama wafanyakazi wa kufagia na kusafisha nyumbani humo wakati wa kutekelezwa kwa wizi huo siku moja kati ya tarehe 1 Desemba na mapema Januari mwaka huu. “Johanne Mapurisa alinunua gari aina ya Toyota Camry… na nyumba ya $20,000 baada ya kisa hicho,” mwendesha mashtaka wa serikali Teveraishe Zinyemba aliambia mahakam...

Poshi: Situmii Mwili Wangu Kutafutia Fedha

Image
NancyTheDreamtz MREMBO Queen Obed ‘Posh Queen’ amefunguka kuwa haamini kuutumia mwili wake kama biashara ili aweze kujipatia fedha kama ambavyo wanavyofanya warembo wengine kwa sababu hata Mungu hapendi. Akizungumza na Ijumaa, Posh alisema mwili na umbo zuri amepewa kama zawadi kutoka kwa Mungu hivyo hawezi kuutumia vibaya kwani atakuwa anamkosea aliyempa. “Kuna watu wengi wananisumbua sana wakijua mimi ni kama wale, hapana, kiukweli ninajiheshimu na watu wanaonifikiria kuwa najiuza hivyo nawaambia kuwa hapa siyo mahali pake kabisa, nimeitafuta elimu ili niweze kupata kazi ya kujikimu maisha yangu mwenyewe,” alisema Posh.

China Waridhia Mkutano wa Pili Kati ya Kim Jong-un na Trump mara ya pili

Image
NancyTheDreamtz Baada ya kutembelea gafla China, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameondoka akiwa anaungwa mkono juu ya uwezekano wa kukutana tena na Rais wa Marekani Donald Trump, televisheni ya taifa iliripoti. Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza mwezi June, lakini maendeleo kuhusiana kuondokana na namatumizi ya nyuklia yalileta matumaini. Rais wa China Xi Jin Ping amesema ana matumaini viongozi hao wawili watakutana nchi yoyote yoyote ambayo si Marekani wala Korea Kaskazini, shirika la habari la Xinhua linaripoti. China ndio rafiki na mshirika mkubwa Korea Kaskazini. Nchi mbili hizo zina mahusiano makubwa na imara ya kibiashara. Xi amesema nchi yake inaunga mkono mkutano wa Korea Kaskazini na Marekani na anaunga mkono pande hizo mbili kujadili tofauti zao kwa mazungumzo. Pia amesema China itakuwa tayari kushika jukumu chanya la kulinda amani na hatimaye kufikia lengo la kuondoa nyuklia katika rasi ya Korea, Xinhua inaripoti. Treni inayoamin...

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Rais Magufuli Kuamuru Kikokotoo cha Zamani Kitumike Mafao ya Wastaafu

Image
NancyTheDreamtz Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe  amempongeza Rais John Magufuli kwa kukubali ushauri walioutoa na kuacha upande wa waziri, washauri wake na watendaji wa Serikali yake. Maoni ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameyatoa leo baada ya Rais Magufuli kurejesha utaratibu wa awali wa kikokotoo cha asilimia 50 kwa watumishi wa Serikali na asilimia 25 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. “Kufuatia uamuzi wa Rais Magufuli kuhusu kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa wastaafu , sisi ACT Wazalendo na vyama vya upinzani kwa ujumla tumesimama na wafanyakazi toka mwanzo wa sakata hili, wakati sheria ikiwa muswada na hata baada ya kanuni kutungwa,” amesema  “Kwetu, jambo lolote linaloongeza maslahi na ustawi wa wafanyakazi ni jambo jema na muhimu. Tunashukuru kuwa Mheshimiwa Rais ametuelewa na amekuja upande wetu na na kuacha upande wa waziri wake, washauri wake na watendaji wa Serikali yake,” ameongeza.  “Tunapoelekea mbele, tunamuomba a...