Diamond Ajibu Mapigo Tuhuma za P Funk Kwa WCB, Atoa Tamko Zito

Diamond Platnumz akiwa na Rayvanny SUPASTAA wa Bongo Fleva ambaye pia ni Mkurugenzi wa lebo ya Wasafi amekanusha tuhuma za kwamba lebo yake inawanyonya wasanii kama inavyodaiwa na baadhi ya watu huku akisisitiza kuwa lebo yake ndiyo inawanyanyua wasanii wadogo kuwainua na kuwafanya kuwa wasanii wakubwa na matajiri nchini. Kauli hiyo ya Diamond inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Prodcer mkongwe wa Bongo, P Funk Majani kudai kuwa WCB inawakadamiza na kuwadhulumu wasanii wake kwa kuwapa mikataba mibovu yenye nia ya kuwadidimiza kimuziki na kibiashara ili WCB ineemeke. Akihojiwa na DW ya nchini Ujerumani, Mondi amesema; “Muziki ni biashara, sisi katika lebo ya WCB tuliwachukua baadhi ya wasanii wakiwa katika makampuni tayari wakifanya kazini, lakini hawakuwa wakubwa, anapokuja kwetu tunawekeza, tunakifanya kile anachokifanya kiwe kikubwa na kiweze kuingiza fedha na awe mkubwa. Ndio maana wasanii wa Wasafi wanakuwa wakubwa sana. “Inapokuja biashara inakuwa kubwa wengi wa vijana wanataka ile biashara iwe yak wake peke yake, ile pesa aikusanye iwe yake peke yake. Wakati ni uwekezaji umefanyika. Akishafikia hapao anaona amekuwa mkubwa anasema mimi nasepa zangu, sasa unasepa vipi wakati ni biashara hii? Watu wamewekeza fedha hapo. P Funk ‘Majani’ Prodyuza mkongwe nchini Tanzania “Mwanzoni watu walikuwa hawafahamu hata upande wa serikali, walidhani wasanii wanaonewa, sio kuonewa, ni biashara, ilifika mpaka kwa Rais na waziri, tukawaeleza wakaona ni kweli. “Ninawekeza zaidi ya Tsh milioni 600, si ningechukua nikaenda kulima hata mahindi. Ninawezeka kwenye kichwa cha sanaanikitegemea nitapata faida ili pesa yangu irudi. “Muziki ukiwa na maneno matupu hauingizi hela, ndio maana wasanii wa WCB wanakuwa wakubwa, wanapata shoo kubwa, wanajiita matajiri kwa sababu wamewekezwa, kwa hiyo unataka ukimbie ili nile hasara? “Wanaosema mikataba ya Wasafi ni ya kikoloni sio kweli, wasanii wa Wasafi wanafedha, nikitoka mimi wanafuata wao, nchi nzima hakuna msanii mwenye pesa kama wasanii wa Wasafi. Zikiwa nyingi unataka ule peke yako hakuna biashara kama hiyo, mimi mwenyewe pesa zangu anakula Tale, Sallam, Fella, ndiyo biashara,” amesema Diamond. Posted by nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele