Posts

Showing posts from July, 2022

Rais Biden Akutwa na Covid-19, Taarifa Yatikisa Ikulu ya Marekani

Joe Biden Rais wa Marekani RAIS wa Marekani Joe Biden ameripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19 hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani. Rais Biden alikuwa tayari ameshatumia dozi mbili za kujikinga na Covid- 19 aina ya Pfizer muda mchache kabla ya kuingia madarakani ambapo chanjo ya kwanza alichanja mwezi Septemba 2021 na ya pili alichanja mwezi Machi mwaka huu. “Asubuhi ya leo Rais Biden amekutwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 na amechanjwa vizuri ingawa amekumbwa na dalili za maambukizi ya virusi hivyo.” Alisema Msemaji wa Ikulu Karine Jean –Pierre. Biden aripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19 Kwa muda mrefu Ikulu ya Marekani imekuwa ikiendesha shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko ya watu pasipo kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Covid-19. Aidha mnamo Aprili 30, 2022 Rais Biden alihudhuria shughuli yenye mkusanyiko wa watu wengi katika Ikulu ya WhiteHouse akiwa hana tahadhari yoyote

Diamond Ajibu Mapigo Tuhuma za P Funk Kwa WCB, Atoa Tamko Zito

Diamond Platnumz akiwa na Rayvanny SUPASTAA wa Bongo Fleva ambaye pia ni Mkurugenzi wa lebo ya Wasafi amekanusha tuhuma za kwamba lebo yake inawanyonya wasanii kama inavyodaiwa na baadhi ya watu huku akisisitiza kuwa lebo yake ndiyo inawanyanyua wasanii wadogo kuwainua na kuwafanya kuwa wasanii wakubwa na matajiri nchini. Kauli hiyo ya Diamond inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Prodcer mkongwe wa Bongo, P Funk Majani kudai kuwa WCB inawakadamiza na kuwadhulumu wasanii wake kwa kuwapa mikataba mibovu yenye nia ya kuwadidimiza kimuziki na kibiashara ili WCB ineemeke. Akihojiwa na DW ya nchini Ujerumani, Mondi amesema; “Muziki ni biashara, sisi katika lebo ya WCB tuliwachukua baadhi ya wasanii wakiwa katika makampuni tayari wakifanya kazini, lakini hawakuwa wakubwa, anapokuja kwetu tunawekeza, tunakifanya kile anachokifanya kiwe kikubwa na kiweze kuingiza fedha na awe mkubwa. Ndio maana wasanii wa Wasafi wanakuwa wakubwa sana. “Inapokuja biashara inakuwa kubwa wengi wa vijana wana

Jinsi masuala ya tehama yalivyofanyika Wizara ya kilimo Dodoma na Nyandiche Technology&Security Services Tanzania Ltd

Ukizungumzia Masuala ya Tehama Tanzania unapaswa kujua kuwa kuna Vijana wanao jitambua ndani ya Nchi hasa katika kutoa huduma zifuatazo:- 1.Elactrical Fence 2.Access Control 3.Cctv Camera 4.Vehicle system 5.Data Entry in system account ackage's 6.Remote Gate 7.Graphics 8.ICT Solutions 9.Video Door Phone 10.Ld Sensor 11.Web Based Data management 12.Printer na Photocopy Repair Shughuli tajwa hapo juu ni kati ya chachu ya kimaendeleo hasa kwa Vijana Tanzania kwa ujumla kwani inatoa ajira timilifu kwa wahusika wa masuala hayo ya Tehama hapa Nchini kwasasa na kwa mfano hapo chini tunakuletea Video za Kijana ajulikanae kama Arthur Raphael Nyandiche akiwa anafanya kazi ya kutengeneza Printer za Wizara ya kilimo Dodoma Prepared by nyandichethedreamtz

Mfahamu Kiundani IGP Mpya Camilius Wambura, Mrithi wa Simon Sirro

Wote tunafahamu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi ambapo amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP akichukua nafasi ya Simon Sirro. Nimejawa na furaha kuona mtu makini ndani ya Jeshi la Polisi mwenye uzoefu na weledi anakabidhiwa majukumu makubwa ya kuliongoza Jeshi letu la Polisi. Hakika CAMILIUS WAMBURA ni mtu sahihi mno. Wengi wetu tunaofuatilia utendaji wa Jeshi la Polisi nchini tulitegemea mabadiliko kufanywa hususani katika nafasi hii muhimu ili kupatikana mtu anayeendana na kasi na dira ya serikali ya awamu ya sita. Baadhi ya nyadhifa na majukumu ndani ya Jeshi la Polisi yaliyowahi kufanywa na IGP CAMILIUS WAMBURA ni pamoja na; 1. Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi – KINONDONI 2. Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi- Makao Makuu 3. Mkurugenzi wa Operesheni-

MANGE Kimambi Amlipua Salama SK Kisa P-Funk Majani, "Umefanya Nini Kwenye Muziki wa Bongo zaidi ya Majungu"?

Ameandika haya Mange Kimambi: Wasafi, Majani ana matatizo yake ila amewaambia ukweli. Na badala ya kumjibu kwa facts nyie mnaenda kwenye personal attacks zinazohusu Harmonize kumtomb** familia yake, ila kipindi kile Ommy Dimpoz alipoongelea kumtomb** Dai mamake mlikasirika sana kwasababu kaingiza mambo ya family. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu…. Alichosema Majani ilibidi kijibiwe kwa facts, Dai mwenyewe alisema kwa mdomo wake kuwa alibeba wimbo wa Mbosso kwenye FOA, je alimpa rights zake juu ya ule wimbo? Naongea sababu kumbukeni Wasafi mliingia mjini kwa kumchafua Ruge Mutahaba kwa kukandamiza wasaniii, haya nyie leo mnafanya nini? Mlivyoingia mjini mlibeba wasaniii woooote wa zamani ambao walikuwa hawaelewani na Clouds,kina Dudubaya sijui nani mkadai hao wasanii walipotea sababu ya Ruge, haya mliishia wapi na wale wasanii? Mbona hamko nao tena? Mlidhani kazi ya kudili na wasanii ni rahisi? Kila msanii wa wasafi akipata jina tu anasepa zake hiyo yote ni sababu ya mkataba m

Simon Msuva "Ninawashukuru Sana Watanzania Wenzangu Niko Tayari Kuanza Upya"

Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva ametoa shukurani kwa wadau wa Soka La Bongo baada ya kukamilisha mpango wa kupata klabu mpya. Msuva amekamilisha usajili wa kujiunga na Al Qadsia ya Saudi Arabia, baada ya kumaliza kesi yake na Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco, iliyoendeshwa na FIFA kwa zaidi ya miezi sita. Kuungo huyo ametumia muda wake kwa kutoa ujumbe mzito wa shukurani kwa Wadau wa Soka La Bongo, kufuatia kuonyesha kuwa naye katika kipindi chote alichokuwa na matatizo. “Naomba nichukue fursa hii kusema asante. Nilipata matatizo na klabu yangu ya hapo awali Wydad Athletic na nilirudi nyumbani kupumzika huku nikiwa nasubiri hatma yangu juu ya matatizo ambayo yaliweza kutokea baina yangu na uongozi wa timu” “Nawashukuru pia Watanzania wote ambao walikuwa pamoja na mimi kwenye kipindi chote kigumu ambacho nilikuwa napitia” “Namshukuru Mama yangu na Baba yangu kwa maneno mazuri yaliweza kunitia nguvu kila niamkapo, bila kusahau familia yangu yote kwa ujumla, mara

Hatimaye Msuva Atimkia Saudi Arabia Kujiunga na Timu ya Daraja la Pili

Winga nyota wa Tanzania Simon Msuva amekamilisha mipango ya kujiunga na timu ya daraja la pili ya AL-QADSIAH. Tayari leo amefanyiwa vipimo vya Afya na vimekwenda vyema. Msuva ambaye alivunja mkataba na miamba ya soka ya Morocco Wydad Casablanca anaanza maisha mapya ya soka Saudi Arabia. nyandichethedreamtz

Diamond athibitisha kununua Ndege binafsi Private Jet

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya WCB Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa ameshanunua Ndege yake yaani Private Jet. Akiongea na DW akiwa nchini Ujerumani Diamond amesema kuwa tayari ameshanunu Ndege ambayo aliwahi kuizungumzia miaka kadhaa sasa na pia meneja wake Sallam Sk ameweka wazi kuwa licha ya Ndege hiyo kununuliwa na Diamond pia itakuwa inatumika kukodishwa. nyandichethedreamtz