Simon Msuva "Ninawashukuru Sana Watanzania Wenzangu Niko Tayari Kuanza Upya"

Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva ametoa shukurani kwa wadau wa Soka La Bongo baada ya kukamilisha mpango wa kupata klabu mpya. Msuva amekamilisha usajili wa kujiunga na Al Qadsia ya Saudi Arabia, baada ya kumaliza kesi yake na Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco, iliyoendeshwa na FIFA kwa zaidi ya miezi sita. Kuungo huyo ametumia muda wake kwa kutoa ujumbe mzito wa shukurani kwa Wadau wa Soka La Bongo, kufuatia kuonyesha kuwa naye katika kipindi chote alichokuwa na matatizo. “Naomba nichukue fursa hii kusema asante. Nilipata matatizo na klabu yangu ya hapo awali Wydad Athletic na nilirudi nyumbani kupumzika huku nikiwa nasubiri hatma yangu juu ya matatizo ambayo yaliweza kutokea baina yangu na uongozi wa timu” “Nawashukuru pia Watanzania wote ambao walikuwa pamoja na mimi kwenye kipindi chote kigumu ambacho nilikuwa napitia” “Namshukuru Mama yangu na Baba yangu kwa maneno mazuri yaliweza kunitia nguvu kila niamkapo, bila kusahau familia yangu yote kwa ujumla, marafiki na watu wote waliokuwa wakiniombea mafanikio juu ya matatizo yangu.” “Mashabiki wangu nawaahidi kuwa nitakuwa nanyi mpaka hatua ya mwisho. Nitawapa furaha nakuonesha uwezo wangu bora kama hapo awali. Nawapenda na nipo tayari kuanza mapambano upya kwenye changamoto mpya” amesema Msuva nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele