Inachekesha..Wamarekani Hawamfahamu Diamond, Wazani ni Mchezaji Mpya wa Timu yao

Baada ya Timu ya @washingtonnfl kumzawadia Jezi na kumpost @diamondplatnumz kwenye page yao ya Instagram, mashabiki wa timu hiyo wameonekana kushangazwa na mtu huyu, huku wengi wakijua ni mchezaji mpya wa timu yao. Maswali mengi yameibuka kutoka kwa mashabiki hao mfano "Who?", "Who is that?" "Can he play" "Can he Help our Team", "Serious Question who is this" Baadhi ya wabongo na waafrika wameonekana kujibu baadhi ya comments za wamarekani kwa kusema kwamba huyu ni msanii kutoka Afrika, East Africa na Wengine wakaitaja Tanzania. Kumbe wasanii wetu Usikute Show zao za marekani huwa wanahudhuria wabongo tu labda na wakenya wa huko, maana hili jambo limeonesha wazi kuwa wasanii kutoka Tanzania hawafahamiki, yani wanajua mchezaji mpya kasajiliwa nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele