Posts

Showing posts from July, 2021

KIINGEREZA cha MTOTO wa SUGU na FAIZA ALLY, ANA AKILI SANA - "NITAKUWA D...

Image

Kaizer Chiefs Vs Al Ahly CAF Champions League Final Livestream TODAY.

Image

Zari Ammisi Diamond Platnumz

Image
B AADA  ya kuachana  na bwana’ke mwingine  aliyepewa jina la Dark  Stallion (Farasi Mweusi),  baby mama wa staa wa muziki  barani Afrika, Nasibu Abdul  au Diamond Platnumz, Zarinah  Hassan au Zari The Boss Lady  amesababisha sintofahamu,  IJUMAA limedokezwa.   Mwanamama Zari ambaye ni  raia wa Uganda mwenye maskani  yake, Durban nchini Afrika  Kusini, amesababisha mjadala  mpya kutoka kwa wafuasi wake  almaarufu Team Zari kwamba ni  rasmi sasa amerejesha majeshi  kwa mwamba Diamond.   ZARI AMEMMISI MONDI? Team Zari wanadai kwamba,  Zari amesababisha mshangao  kwao baada ya kudaiwa kummisi  Diamond au Mondi; muda mfupi  baada ya kumwagana na huyo Dark  Stallion ambaye jina lake halisi  ni Frederick Nuamah, mwigizaji  na prodyuza mkubwa wa filamu  nchini Ghana. Zari ambaye ni mama wa watoto  watano, anasema kuwa, anammisi  mtu f’lani ambaye Team ...

Deus Kaseke Asaini Miaka Miwili Yanga

Image
KATIKA kuhakikisha wanakiboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, Yanga imemuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo Deus Kaseke. Huyo atakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba.   Kaseke ni kati ya wachezaji kipenzi cha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ambaye tangu akabidhiwe kikosi hicho amekuwa akimtumia nyota huyo katika kikosi cha kwanza. Huyo anakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba Yanga kati ya hao ambao mikataba imemalizika, mwingine ni Mapinduzi Balama.   Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Yanga hivi sasa inafanya usajili wake kwa usiri mkubwa na tayari imewaongezea mikataba wachezaji wake ambao Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi amewapendekeza.   Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya wachezaji waliongezewa mikataba yupo Kaseke ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.Aliongeza kuwa tofauti na wachezaji wanaoongezewa mikataba, pia mabosi wa timu hiyo wanaendelea na usajili mpya wa kitaifa na kimataifa. ...

Timu ya kushabikia Katika fainali ya EURO 2020

Image
Italia au England ni nani atainua kombe hilo Katika fainali ya UEFA EURO 2020 kwenye Uwanja wa Wembley mnamo Julai 11? Je! Unatafuta timu ya kuishabikia katika michuano hiyo ya fainali? Au unatafuta timu ya kitaifa iliyo na wachezaji kutoka klabu unayoipenda? Ikiwa unatamani kushabikia timu ambayo itaendana na mawazo yako, soma mwongozo wetu kwa waloingia fainali. Uingereza Ikiwa unapendelea sana Magoli basi Uingereza ni chaguo linalokufaa kutokana na magoli ambayo wameyafunga katika kufuzu kwao. Vijana hawa wa  Gareth Southgate pia wanacheza EURO yao ya kumi na ndio timu ya taifa iliyocheza sana katika michuano hiyo ya EURO bila ya kunyakua taji hilo. je! Wakati wao umefika wa kunyakua taji hilo kwa mara ya kwanza tangu Kombe la Dunia la FIFA mnamo 1966? Italia Unafurahishwa na mchezo wa mikwaju ya penati? Ikiwa ndivyo, Italia ndio timu inayokufaa kwani wamehusika katika rekodi ya mafanikio makubwa sana katika upande wa penati ikiwemo ushindi wao wa nusu fainali dhidi ya Uhispania...

Kumbe Yawezekana Kuhititimsha Chuo Ukiwa Bikira na Mpaka Kuolewa

Image
Watu daima wanafikiria kuwa kuhitimu kutoka chuo kikuu kama bikira haiwezekani. Wengine wanasema kuwa bikira husababishwa na ukosefu wa nafasi au fursa; vizuri kwa upande wangu haikuwa kamwe kwa sababu ya ukosefu wa fursa lakini nidhamu.Wakati nilikuwa shule ya upili, karibu marafiki wangu wote walikuwa na marafiki wa kiume ambao walijisifu wakati mwingi. Nilihisi isiyo ya kawaida nje na nililazimika kuwa nayo lakini sio. Haikuwa kwa sababu sikuwa na hamu, lakini kwa sababu ya malezi yangu. Niliogopa na zaidi ya hayo, sikutaka kufanya chochote ambacho kitaleta aibu  kwa familia yangu. Wazazi wangu kamwe hawakutaka hii iwe sehemu ya binti yao. Nilihitimu kutoka Shule ya Upili mnamo 2018 na kisha nikaandikishwa katika moja ya chuo kikuu mashuhuri nchini Kenya. Chumba mwenzangu alikuwa kinyume kabisa na mimi mwenyewe, anafurahia kwenda kwenye sherehe, vilabu, kunywa pombe na mikusanyiko mingine ya kijamii.Wakati mwingine, nikalazimika kutoka nje ya chumba kwa sababu analeta mpenzi wak...

Nay wa Mitego amchana Fred Vunja Bei amuita mshamba wa wanawake 'Walikuwepo kama yeye wamefilisika'

Image
Nay wa Mitego amchana Fred Vunja Bei amuita mshamba wa wanawake 'Walikuwepo kama yeye wamefilisika' VIDEO: nyandichethedreamtz

HAMISA afunguka kuhusu mahusiano yake na RICK ROSS kwa mara ya kwanza, Kuhamia Marekani, NGOMA mpya

Image
HAMISA afunguka kuhusu mahusiano yake na RICK ROSS kwa mara ya kwanza, Kuhamia Marekani, NGOMA mpya VIDEO: nyandichethedreamtz

Chidi Benz: Tumefanya Vanessa Kauchukia Muziki

Image
Ni maoni ya msanii wa HipHop, Chidi Benz ‘King Kong’ kuhusu suala la Vanessa Mdee kutangaza kuachana na masuala ya muziki ambapo anadai watanzania ndio wamemfanya msanii huyo kuuchukia muziki.   Chidi Benz ametoa comment yake hiyo kupitia page yake ya Instagram baada ya kumpost Vanessa Mdee kisha kuandika; “Sema Tanzania nayo, from no where tumefanya my sister Vannesa Mdee kauchukia muziki, Ilikua tunahitaji sana vitu kutoka sauti ile, sijui wengineo.”   Siku za hivi karibuni msanii huyo wa HipHop amekuwa akitoa maoni na mitazamo kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu masuala mbalimbali ya muziki, wasanii na tuzo. nyandichethedreamtz

Waziri Simbachawene aruhusu Polisi kuhamia nyumba mpya Dar

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, George  Simbachawene ameruhusu askari wa polisi na maofisa wa jeshi hilo kuanza kuishi katika nyumba za kisasa za maghorofa pacha 11 na 23 zilizopo maeneo ya Mikocheni na  Kunduchi wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam. Mradi wa nyumba hizo ambazo familia 330 zinaweza kuishi, ujenzi wake ulikamilika miaka mitatu iliyopita lakini hazikuanza kutumika kwa sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kisera. Simbachawene ametoa ruhusa hiyo leo Ijumaa Julai 9, 2021  alipotembelea mradi wa nyumba hizo zilizojengwa  na kampuni ya Mara World Tanzania Ltd. Katika maelezo yake, Simbachawene alimuagiza mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( IGP), Simon Sirro kuhakikisha askari hao waingia mara moja katika nyumba huku taratibu za kisheria zikiendelea kutatuliwa kati ya Serikali na mwekezaji. Uamuzi huo ulipokelewa kwa furaha na IGP Sirro ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa akiiangukia Serikali kuruhusu nyumba hizo kuanza kutumika ili askari watekeleze...

P Diddy Ashusha Tuhuma Nzito Kwa Wazungu

Image
Baada ya mwanariadha Sha’Carri Richardson kuenguliwa kwenye mbio za Mita 100 kwenye michuano ya Olimpiki 2020 ambayo itaanza Julai 23, mwaka huko Tokyo, Japan na sababu kuu ya kuenguliwa kwake ikiwa ni baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa anatumia bangi, rapa P Diddy wa Marekani ameshusha tuhuma nzito dhidi ya wazungu.   P Diddy amesema anakerwa na watu mbalimbali hasa wazungu ambao wamekuwa wakimnanga Sha’Carri mitandaoni akiwemo mwandishi mmoja kutoka Australia ambaye alikwenda mbali zaidi na kudai mwanadada huyo ni feki kama zilivyo nywele na kucha zake.   P Diddy kupitia ukurasa wake wa Instagram anawalaumu wote wanaomnanga mwanadada huyo na kusema kuwa bangi haimfanyi mtu awe na mbio zaidi kama baadhi ya watu wanavyodhani kuwa mwanadada huyo amekuwa akishinda kutokana na kutumia bangi.   P Diddy ameshusha shutuma nzito kwa wazungu akisema kuwa amechoka kuwaona wazungu wanakaa na kutunga sheria ngumu ambazo ni kwa ajili ya kuharibu na kudidimiza ndoto na maleng...