Nawakumbusha Wanaharakati wa Twitter Kuwa Huwezi Kuua Mziki Mzuri, Kujaribu Kumshusha Diamond Platnumz ni Uzuzu

 


Niko Ulaya na nimeshuhudia popote panapopigwa muziki wa afropop basi ni Nigeria, South Africa, DRC na Tanzania, nikisema Tanzania basi ni muziki wa Diamond Platnumz au kundi zima la WASAFI.

Mwaka 2017 nilikuwa Nairobi na kwenda club ambapo nilishuhudia karibu 90% ya muziki uliokuwa unapigwa basi ulikuwa ni wa Diamond ama msanii wa kundi lake, wakizidi sana walikuwa wanapiga muziki wa Nevy Kenzo "kamatia chini".

Ni akili iliyojaa matope tu kujaribu kuzuia nyota wa pop wa Tanzania Diamond Platnumz eti asishinde tuzo za BET2021 eti kwa sababu aliiunga mkono CCM kwenye uchaguzi wa 2020.

Huyu kijana nyota licha ya kwamba ana kipaji ni mtu mwenye juhudi zisizo na mfano hasa ukichukulia kwamba anatoka nchi iliyojaa vijana wavivu wa kufikiri na wasio na juhudi ya kutafuta mali.

Diamond Platnumz ameajiri vijana wengi sana na hivyo kuboresha maisha ya watanzania wengi bila ya kujali itikadi zao.

Diamond ni mfanya biashara hivyo hachagui afanye kazi na nani, hata siku CHADEMA wakija na pesa ndefu kwa nini asimuimbie Mwenyekiti Mbowe, kamanda wetu asiyetetereka?


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele