Kajala: Paula Anakwenda Shule

STAA mkali wa Bongo Movies, Kajala Masanja, amevunja ukimya uliotawala kwa kipindi kirefu baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’; kubwa ni suala la mwanawe, Paula Paul au Paula Kajala kwenda shule.

 

Kajala anasema kuwa, kwa sasa yupo fiti na anaendelea vyema na maisha yake kama kawaida.

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Kajala ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Paula anasema amekutana na changamoto nyingi ndani ya mwaka huu na kamwe hawezi kuja kusahau ambapo amejifunza mambo mengi maishani mwake.

 

Kajala anasema kuwa, yeye pamoja na mtoto wake, Paula wamejifunza mengi ambayo hawatayasahau.

KWANI KAJALA MWENYEWE ANASEMAJE?

 

IJUMAA: Habari za siku kedekede Kajala…

 

KAJALA: Salama kabisa…

 

IJUMAA: Pole na misukosuko ya hapa na pale.

 

KAJALA: Asante sana, nashukuru Mungu mambo yamepita na kila linalonijia nalipuuzia tu.

 

IJUMAA: Mambo ni mengi ambayo yemetokea maana likitoka hili linaingia lingine, hali hii umeichukuliaje?

 

KAJALA: Katika maisha yetu ya kila siku huwezi ‘kumplizi’ kila mwanadamu, utamuacha aseme kwa sababu ukweli unaujua.

 

IJUMAA: Kipindi chote cha maumivu, tena ukiunganishwa na mtoto wako, Paula vipi kwa upande wa Paula, unamuathiri vipi?

 

KAJALA: Tena huwezi kuamini, yeye ndiye ananipa sana moyo mimi kwa kila kitu, ananiambia; ‘mama kama wewe ndiye unaujua ukweli ndani ya moyo wako, kwa nini mwanadamu akusumbue?’

 

IJUMAA: Vipi kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ziliwaweka kwenye wakati gani?KAJALA: Lazima uumie kwa sababu mtu anakusingizia kitu kikubwa kama hicho, lakini siku zote penye ukweli uongo ujitenga na Mungu amezidi kutupa ujasiri.

 

IJUMAA: Watu wengi wanasema kuwa Paula ndiyo hawezi kwenda shule tena kwa sababu tayari wanaotakiwa kwenda kidato cha tano wamechaguliwa na hakuna jina lake, hili nalo likoje?

 

KAJALA: Anakwenda shule kwa sababu shule zipo nyingi tu za kidato cha tano na sita na atawashangaza wengi darasani.

 

IJUMAA: Naelewa wazazi wako wote wapo, wanachuliaje hii misukosuko unayokutana nayo?

 

KAJALA: Yaani bora hata baba yangu anaweza kuelewa, lakini mama yangu kila siku ni kulia tu.IJUMAA: Umewahi kujuta kuwa staa?

 

KAJALA: Hata Paula ametoka kuniambia hivi karibu kuwa anajuta kuwa staa, kwa kweli mambo ni mengi sana.

 

IJUMAA: Sasa hivi inaonekana kila sehemu unapokwenda unakuwa na Paula, ndiye amekuwa rafiki wako wa sasa?

 

KAJALA: Mimi sina rafiki zaidi ya Lamata (prodyuza wake) hivyo Paula ndiye mtu wangu wa karibu siku zote.IJUMAA: Bado unampiga Paula anapokosea?

KAJALA: Paula ni msichana mkubwa sasa, tunakaa na kuzungumza.

 

IJUMAA: Huna mpango wa kumuongezea mdogo wake?

 

KAJALA: Mpango huo upo.

 

IJUMAA: Ukiacha mambo mengine, Paula ni mtoto wako, ana nini cha zaidi kwako?

 

KAJALA: Paula ni moyo wangu, furaha yangu na kila kitu.

 

IJUMAA: Haya, asante sana kwa ushirikiano wako Kajala, Gazeti la IJUMAA linakutakia kila la heri.

KAJALA: Asante sana na karibu tena.

NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele