BINGWA mtetezi wa ligi kuu Simba, leo Juni 19, imefanikiwa kuvuna alama tatu, dhidi ya Polisi Tanzania, kwenye mchezo  uliochezwa katika  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kushinda bao 1-0.

 

Goli pekee la kwenye mchezo huo limefungwa na Luis Miquissone dakika ya 28 kwa adhabu ndogo (Free kick) baada ya beki wa kulia Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi nje ya 18, bao hilo la nane kwenye ligi kuu kwa ‘Konde Boy’

 

Kwa matokeo hayo Simba ambaye ni bingwa mtetezi wa ligi imefikisha alama 70, baada ya kushuka dimbani mara 28, nafasi ya pili ipo Yanga yenye alama 64,  baada ya kucheza michezo 30.

 


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele