Posts

Showing posts from June, 2021
Image
BINGWA mtetezi wa ligi kuu Simba, leo Juni 19, imefanikiwa kuvuna alama tatu, dhidi ya Polisi Tanzania, kwenye mchezo  uliochezwa katika  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kushinda bao 1-0.   Goli pekee la kwenye mchezo huo limefungwa na Luis Miquissone dakika ya 28 kwa adhabu ndogo (Free kick) baada ya beki wa kulia Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi nje ya 18, bao hilo la nane kwenye ligi kuu kwa ‘Konde Boy’   Kwa matokeo hayo Simba ambaye ni bingwa mtetezi wa ligi imefikisha alama 70, baada ya kushuka dimbani mara 28, nafasi ya pili ipo Yanga yenye alama 64,  baada ya kucheza michezo 30.   NancyTheDreamtz

Kajala: Paula Anakwenda Shule

Image
S TAA  mkali wa Bongo  Movies, Kajala Masanja,  amevunja ukimya  uliotawala kwa kipindi  kirefu baada ya kuachana na  aliyekuwa mpenzi wake ambaye  ni msanii wa muziki wa Kizazi  Kipya, Rajab Abdul Kahali  ‘Harmonize’; kubwa ni suala la  mwanawe, Paula Paul au Paula  Kajala kwenda shule.   Kajala anasema kuwa, kwa  sasa yupo fiti na anaendelea  vyema na maisha yake kama  kawaida.   Katika mahojiano maalum  (exclusive interview) na Gazeti la  IJUMAA, Kajala ambaye ni mama  wa mtoto mmoja, Paula anasema  amekutana na changamoto  nyingi ndani ya mwaka huu na  kamwe hawezi kuja kusahau  ambapo amejifunza mambo  mengi maishani mwake.   Kajala anasema kuwa, yeye  pamoja na mtoto wake, Paula  wamejifunza mengi ambayo  hawatayasahau. KWANI KAJALA MWENYEWE  ANASEMAJE?   IJUMAA:  Habari za siku  kedekede Kajala…   KAJALA:  Salama...

Rais Samia Ateua Wakuu wa Wilaya Wapya-Video

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Juni 19, 2021 mefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara.                 NancyTheDreamtz

Video: Meja Kunta Afanya Balaa Nandy Festival Mwanza

Image
MWANAMUZIKI anayefanya poa kwenye muziki wa Singeli Bongo, Khalid Sadick ‘Meja Kunta’  amefanya balaa usiku wa kuamkia leo Juni 18, 2021 jijini Mwanza kwa kupiga shoo ya nguvu kwenye Tamasha la Nandy Festival. NancyTheDreamtz

Nandy Festival 2021; Ben Pol Apiga Shoo ya Kibabe Mwanza – Video

Image
MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva, Benham Paul ‘Ben Pol’, usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2021 amefanya shoo ya aina yake jijini  Mwanza  kwenye tamasha lake la Nandy Festival 2021. Nandy, amesindikizwa na wanamuziki wengine akiwemo Baba Levo, Fid Q, Meja Kunta na wengine.  NancyTheDreamtz

Breaking: Papa Msofe Afutiwa Mashtaka, Aachiwa Huru

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 18, 2021 imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara  Marijan Msofe (53) maarufu Papa Msofe na wenzake wanne.   Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo akieleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao. Msofe na wenzake walikuwa wanakabiliwa wa mashtaka matano likiwemo la kujipatia Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu.   Mbali na Papa Msofe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 124/2019 ni Wenceslaus Mtu(49), Mwesigwa Mhingo (36), Josephine Haule (38) na Fadhil Mganga (61).   Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa hao umetolewa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Awali, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa DPP ameieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo. Baada ya upande mashtaka kueleza hiyo, Shai...