Picha: Askofu T.D Jakes wa kanisa la Potters Marekani awasili nchini Kenya

Askofu, mjasiriamali, muandishi na muigizaji maarufu wa Marekani yupo nchini Kenya. TD Jakes ambae ni maarufu sana duniani kwa safu za sinema, uandishi wa vitabu vya kutia motisha mbali na mahubiri yanayofatiliwa na wafuasi wengi zaidi duniani, amealikwa Kenya na kampuni ya utalii ya Bonfire Adventures ambayo imekua ikifanya kazi kwa karibu na mastaa wengi nchini Kenya kuhakikisha inatangaza utalii.
Askofu TD Jakes Katikati akikabidhiwa Tembo na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Bonfire Adventure

Kupitia ukurasa wao wa Facebook, kampuni hii imetupia picha ya Askofu TD Jakes akiwa kwenye mbuga ya wanyama na akiwa amezingirwa na wafanyikazi wa kampuni hii huku habari za ndani zikidhibitisha kua TD Jakes amekabidhiwa Tembo ambae mamake aliuawa na wawindaji haramu. Safari hii ambayo imegaramiwa na Bonfire Adventures niyakurudisha rasmi shughuli za kampuni hiyo ambayo iliathirika sana na kufungwa kwa safari za ndege kote duniani kwa athari za ugonjwa wa COVID19.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais