Timu Samatta Yachapwa Mabao 3-1 Na Timu Kiba, Morrison Akosa Penalti


TIMUKiba leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya TimuSamatta kwenye mchezo wa hisani wa SamaKiba Foundation uliochezwa Uwanja wa Mkapa.



Lengo la mchezo wa leo ni kurejesha kile wanachokipata kwa jamii ambapo mchezo wa leo ulikuwa ni wa tatu kwa TimuKiba na TimuSamatta kukutana huku mechi zote mbili zilizopita ushindi ulikuwa ni kwa TimuSamatta hivyo leo TimuKiba imepata ushindi wa kwanza.


Mabao ya upande wa TimuKiba yalifungwa na Ibrahim Ajibu  dakika ya 25,Mudhathir Yahya dakika ya 53 na la tatu lilipachikwa na Hassan Dilunga dakika ya 90.

Bao pekee la TimuSamatta lilifungwa na Yahaya ambaye alijifunga dakika 59.


TimuSamatta walipata penalti mbili zote zilipigwa na Bernard Morrison ambaye alikosa penalti ya kwanza baada ya kumpa pasi Idd Naldo aliyepaisha na ile ya pili Morrison aliipaisha mwenyewe.

Kiba amesema kuwa ni furaha kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi huku akiwaomba waendelee kutoa sapoti.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais