Papa Francis awateuwa wanawake sita kusimamia fedha za Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amewateuwa wanawake sita, akiwemo mweka hazina wa zamani wa Mwanamfalme Charles wa Uingereza, kuhudumu katika baraza linalosimamia fedha za Vatican.
Uteuzi huo kwenye mojawapo ya ofisi muhimu kabisa za Makao makuu ya kanisa hilo unadhihirisha jitihada ya karibuni ya papa Francis kutimiza ahadi za kuimarisha usawa wa kijinsia alizotoa miaka kadhaa iliyopita lakini wanawake wakasema zilichukua muda mrefu sana kutimizwa.
Francis tayari aliwateuwa wanawake kuwa naibu waziri wa mambo ya kigeni, mkurugenzi mkuu wa Majumba ya Makumbusho ya Vatican, na naibu mkuu wa Ofisi ya Habari ya Vatican, pamoja na wanawake wanne kama wanachama wa Baraza la Maaskofu, ambalo huandaa mikutano mikuu.
Comments