Afrika Kusini ndio taifa lililoathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya covid-19
Idadi ya watu ambao wamekwishaambukiwa virusi vya corona ulimwenguni, idadi yake imefikia watu milioni 18,7 huku idadi ya watu waliofariki ikiripotiwa kufikia watu 704 632.
Idadi ya jumla ya watu ambao wamekwishapona vilevile baada ya kupatiwa matibabu inaendelea kuongezeka, idadi hiyo imefahamishwa kufikia watu zaidi ya milioni 11,9 kote ulimwenguni.
Ndani ya masaa 24 nchini India , watu 904 wamefariki kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Vifo hivyo ambavyo vimetokea ndani ya masaa 24 vimepelekea idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutomana na maambukizi ya virusi hivyo kufikia watu 40 772.
Idadi ya watu ambao wamekwishaambukiwa covid-19 nchini India inaripotiwa kufikia watu milioni 1,9.
Katika jimbo la Gujarat, ajali ya moto iliotokea katika hospitali moja imepelekea vifo vya watu wanane.
Nchini Urusi, watu 14 606 wamekwishafariki huku watu 871 894 wakiwa na maambukizi.
Nchini Iran ni watu 17 802 ndio ambao wamekwishafariki kwa virusi hivyo huku idadi ya watu walşoathirika na maambukizi ya covid-19 ikiripotiwa kuwa watu 317 483.
Nchini Pakistani, watu 6035 wamefariki, nchini Indoneaia watu 5 452 wamefariki, nchini Irak watu 5 094 na nchini Saudia ni watu 3020 ndşo ambao wameripotiwa kufariki.
Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kwa covid-19 barani Afrika imefikia watu 21 679.
Idadi kubwa ya watu waliofariki kwa covid-19 barani humo inapatikana nchini Afrika Kusini ambapo watu 9298 wamefariki.
Nchini Misri ni wa 4930 na nchini Algeria ni watu 1261 ndio waliofariki kwa maambukizi hayo.
Comments